Pasipo Utakatifu, hakuna atakayemuona MUNGU

na Mwl Abel Suleiman Shiriwa


Wapendwa katika BWANA, tusidanganyane, pasipo Utakatifu, hakuna atakayemuona Mungu"  Waebrania 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo
Utakatifu ambao hapana mtu atakayemuona BWANA asipokuwa nao.


Kwa hivyo Utakatifu ndiyo nguzo muhimu itakayomfanya kila Mtu mwenye nao amuone MUNGU, kwani unapotaka kuwa Karibu na MUNGU, ni Lazima
Ujitakase.

Walawi 20:7 Jitakasaneni basi, iweni Watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

"Na hauwezi kuwa Mtakatifu pasipo kuzishika Sheria na Amri za MUNGU"

Walawi 20:8 Nanyi zishikeni Sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.

"Vile vile huwezi kuzishika Amri za MUNGU, ambazo zitakufanya Uwe
Mtakatifu, bila kuwa na Upendo"

Yohana 14:15 Mkinipenda Mtazishika Amri zangu.

"Kwa hivyo ni lazima Utangulize Upendo, maana ukiwa na Upendo, Utashika
Amri za MUNGU, na ukishika Amri za MUNGU, utampendeza MUNGU, kwani
utajua MUNGU anataka ufanye nini, na hataki ufanye nini, ndiyo maana
YESU KRISTO akasisitiza Upendo kwa Wanafunzi wake"

Yohana 13:34-35 ''Amri mpya nawapa, Mpendane kama vile nilivyowapenda ninyih nanyi
mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watambua ya kuwa ninyi mmekuwa Wanafunzi wangu, mkiwa na Upendo ninyi kwa ninyi.


"Kwa hivyo tunapaswa sana sisi Wakristo wote, kuwa na Upendo sisi kwa
sisi, maana sote ni ndugu.

1 Yohana 4:20-21 ''Mtu akisema, Nampenda MUNGU, naye amchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa Maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona hawezi kumpena MUNGU
ambaye hakumwona.Na amri hii tumepewa na yeye ya kwamba ampendaye MUNGU, ampende na ndugu yake.


"Kwa hivyo huwezi kujiita Mtakatifu, hali ya kuwa unamchukia ndugu yako"

1 Yohana 3:15 Kila amchukue ndugu yake ni Mwuaji, nanyi mnajua ya kuwa
kila Muuaji hana Uzima wa Milele ukikaa ndani yake.

Tusiwe na Upendo wa Msimu, bali Upendo wa Kudumu.

Waebrania 13:1-3'' Upendo wa ndugu na udumu. Msisahu kuwafadhili wageni; kwa maana kwa njia hii wengine
waliwakaribisha Malaika pasipo kujua. Wakumbukeni hao waliofungwa kama mmefungwa pamoja nao, nao
wanaodhulumiwa kwa vile ninyi mlivyo katika Mwili.


Vile vile, katika Kupenda kwetu, tusiwe na Pendo la Kinafiki.

Warumi 12:9 Pendo lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, Mkiambatana
na lililo Jema.


Tunapaswa kuwapenda pia na Adui Zetu.
Luka 6 27-28 ''Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia, Wapendeni Adui zenu, watetendeeni
mema wale ambao wawachukia ninyi. Wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.''

Upendo unachukua Mambo mengi sana,
 1Korintho 13:1-8 ''Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za Malaika kama sina upendo,
nimekuwa kama shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na Maarifa yote,
nijapokuwa na Imani tilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina
upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu kuwalisha Masikini, tena nikijitoa mwili wangu uungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo huvumilia, Hufadhili; Upendo hauhusudu; Upendo hautakabari: haujivuni: Haukosi kuwa na adabu; hautaufuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya. Haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; Huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote. Upendo haupungui Neno wakati wote...


Najua Somo la Upendo ni pana sana, kiasi Kwamba, huwezi kuliandika
ukamaliza, ila kwa Kichache hiki, nimeona Vema, Ku-share, pamoja nanyi.

MUNGU awabariki sana
 By
Mwl Abel Suleiman Shiriwa

Comments