NGUVU YA IMANI:


Imani ni mkono wa mwanadamu unaonyooshwa kupokea kutoka kwa Mungu. Ambao ukishapokea huitwa Neema. Lakini ili upokee lazima uwe na mkono wa Imani.
1. Haiwezekani kupendeza kama huna Imani. Efeso 2:8.''

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; Imani na Neema vinatembea pamoja.

2. Katika safari ya maisha ya mwanadamu anahitaji Imani ili tuende Mbinguni.1PETRO 1:5.
Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.
3. Ukiamini utauona wokovu wa Mungu. Ebrania 11:4.

Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.
4. Kila jambo linatanguliwa na Imani. Ebrania .11:32-33.

Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, 
 
5. Watumishi wa Mungu Shedrabk, Meshak,na Abednego baada ya kukataa kuiabudu Sanamu wakasema Mungu wetu aweza kutuokoa lakini hata asipotuokoa na moto basi tuko tayari kufa. Lakini Wayahudi wengine waliochukuliwa mateka walikubali kuungana na watu wengine kuabudu Sanamu ya Mfalme.Danieli 3:12-30

Katika Imani hatupaswi kuangalia nani atafanya nini, hatupaswi kufata mkumbo lakini tuyaangalie maagizo ya Mungu yanasema nini na tuyatende kwa gharama yoyote usikengeuke kulia wa lakushoto usitende dhambi na kuharibu mpango wa Mungu na hatimaye Mungu atakuokoa.

Comments