NILIWAHI KUWA USO KWA USO NA MALAIKA MWENYE PANGA LINALOWAKA MOTO

Ndugu ubarikiwe na hongera kwa kuifanya kazi ya Mungu
kwa ufasaha. Mimi ni mzaliwa wa kijiji cha Nyakahula huko Kagera japokua kwa sasa naishi Bagamoyo kabila langu ni mhangaza na umri ni miaka 51. na kwa bahati mbaya sana nilijiingiza udokozi na baadae wizi kabisa tena uliokubuhu, ilikua rahisi sana kuanza wizi japokua ilikua ni vigumu sana kuacha tabia hiyo isiyotakiwa na serikali hadi wanadamu wote. na mwanzoni sikuwa na tabia hiyo ila rafiki yangu mmoja ambaye kwa sasa ni marehemu ndio aliniunganisha na kikundi cha vijana wenzangu ambao walikua wanajishughurisha na ununuaji wa mahindi kijijini kwetu na vijiji jirani ambapo na mimi nilijiunga kufanya biashara hiyo na kuna jambo la siri ambalo sikulijua ila siku chache tu baada ya kujiunga kwenye kikundi hicho kwa msaada wa rafiki na tabia hiyo tulikua na tabia ya kununua mahindi mchana na usiku tunaenda kuwavamia wale wale ambao tulinunua mzigo kwao tena na mara nyingi sana tulikua na tabia ya kununua mahindi mengi kwa mtu mmoja ambapo usiku wa siku hiyihiyo au kesho yake tulikua tunaifata pesa yetu kwa njia ya wizi maana tulikua na uhakika kwamba kuna pesa shilingi ngapi. wizi ulipamba moto sana na ajabu kuna siku nusura nife baada ya mwenzangu mmoja kupigwa na mshale na kufa hapo hapo na kwa sababu alikua jirani sana na mimi nilibahatika tu na tukatoroka na kukimbia wilaya nyingine kwa kudhani kuwa mwenzetu aliyepigwa na mshale ametutaja kumbe alikufa kabla hajatutaja na hiyo tuliijua baada ya miezi kadhaa kupita. licha ya kuwa wilaya jirani na pale tulipokua tuliendelea na wizi na kwa wakati huo tuliacha wizi wa staili ya kwanza na kuanza kujificha karibu karibu na mto na kusubiria yeyote atakayepita usiku tunamkaba na kumchukulia pesa na kumbuka kuwa kipindi hicho cha 1988-1991 hapakua na simu hivyo cha muhimu cha kuchukua ilikua na pesa. siku moja ambayo sitaisahau maishani mwangu na ilikua siku ya ijumaa tulikua pale kwenye kidaraja mida ya saa mbili usiku alipita pinti mmoja ambaye tulikua tunamfahamu na tulijua alikua anakwenda kanisani kwenye mkesha maana  maana alikua ni mwanakwaya na ukivuka daraja kuna kanisa, Tulimwacha dada huyo apite lakini tuliapa kumbaka wakati akirudi kutoka kanisani maana kwa miezi kama miwili tulikua tunamwacha tu kila ijumaa apite. siku hiyo hatukupata mteja au mtu wa kumkaba na kuchukua pesa na tuliendelea kukaa pale hadi saa kumi na nusu asubuhi yule binti tulimwona yule binti akija pole pole huku akiimba pambio na naikumbuka sana maana alikua anaimba kwamba NINAYE YESU NIMEHAKIKISHA, KAMANDA WANGU NITASHINDA VITAAA. alipokaribia tulijigawa na kumzunguka nyuma na mbele na kwa kweli siku hiyo tungembaka hadi kumwua maana watu 4 wote tulikua tumepanga kufanya unyama huo, aliposogea zaidi tulijitokeza na kumkamata na mimi ndiyo ilitakiwa niwe wa kwanza kumbaka maana mwanzo tulikua tumeshapiga kura ili kubaini nani aanze na nani afuate na hadi nani awe wa mwisho.tulimkamata na kumwangusha chini na wakati mimi najiandaa kumbaka nikiwa bado hata nguo sijavua ulitokea mwanga mkali sana kama radi jirani tu na tulipokua yaani ni kama umbali wa mita 25 na tulipoangalia vizuri tulimwona mwanaume anayeng'aa sana na mikono yake yote miwili alikua ameshika panga ndefu sana mikononi mwake na panga ili ilikua inatoa moto japokua haukua mwingi sana. na kwa kweli kila mmoja alijua kuwa yule hakuwa mwanadamu wa kawaida ila alikua ni malaika na kwa kweli nilijikuta nakimbia ghafla huku napiga kelele maana nilijua kifo kilifika na kwa habari za wenzangu watatu hata sikujua walikoelekea. nilikimbia hadi kijiji jirani na sikujua yaliyoendelea na tangu siku hiyo niliacha wizi na nikagundua hakika watu wanaomtegemea Mungu kwa asilimia 100% hakika yeye huwalinda. kwa bahati nzuri baada ya muda mrefu yule dada siku moja nilimwona sokoni na nikajikuta namwangalia sana na kwa kweli nilishindwa kujizuia nikamwuliza ambapo alinishangaa sana ila akaniambia kuwa yeye hakuona chochote ila aliona tu tukikimbia na yeye akaanza kuogopa akidhani kuna simba ila baada ya muda akawa na amani na akasikia sauti ikimwambia BINTI NENDA MYUMBANI MIMI NI MALAIKA NIMETUMWA KUJA KUKUOKOA NA KIFO, NA ENDELEA NA JUKUMU LAKO KANISANI.nilishangaa sana kwamba binti yule hakumwona yule malaika na ule mwanga ambao hata kama ukiwa mita 500 ungeuona, nilimwomba msamaha sana na akaniambia niokoke na kuondoka. kwa keili tukio hilo la malaika bado nalikumbuka sana na baadae kwa kutafuta maisha nilihamia mikoa ya pwani yaani morogoro hadi sasa niko bagamoyo. niombee sana  japokua niliacha wizi tangu mwaka 1992 lakini nimeshindwa kuokoka japokua MUNGU akipenda mwakani nitaokoka rasmi.

Kutoka Maisha ya ushindi blog

ndugu nafasi ya wokovu ni sasa na kwa ushauri wangu nakuomba uokoke leo maana hakuna ajuaye yatakayojiri kesho na utapokea uponyaji wa roho na mwili (Mathayo 11:28)

Comments

Unknown said…
Anapaswa kuokoka kwakweli, tena asisubiri mwakani, aamue sasa
Peter Mabula said…
kweli kabisa mtumishi maana wokovu ni sasa wala sio mwakani. ubarikiwe sana pia maana atakaposoma msisitizo wako ataamua vyema maana maamuzi ya leo ndiyo matokeo ya kesho hivyo ni heri kuamua vyema leo