NJOO KWA YESU,UONE RAHA MWENYEWE



Njooni kwangu ninyi nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha. (Mathayo 11:28).

Wewe unaesumbuliwa na magonjwa, laana,mateso mbalimbali,kutaliwa,njoo kwa Yesu upate pumziko. Uliyetengwa na ndugu,rafiki,jamaa,njoo kwa Yesu,yeye anakupenda bado.Isikie sauti hii; Ulitingwa na masomo,hufanikiwi katika kazi zako,masomo yamekuwa mlima mbele yako, sauti ya Yesu
inakuita sasa,chukua hatua,uje kwa Yesu upate pumziko.

Haijalishi, umefunga na kuomba mara ngapi,pengine hata umekata tamaa kuwa Mungu hajajibu maombi yako,lakini sasa,isikie sauti hii,Mungu amesikia kilio chako. Wewe uliye mjane,uliyesongwa na madeni, ulevi umekushinda,sigara zimekushinda, umeshindwa kusamehe waliokukosea, eti kisa hawajakuomba msamaha, jiachilie kwa Yesu, njoo upumzike.

Uliyefunga kufuli la visasi,chuki na hasira moyoni mwako, njoo kwa Yesu upumzike,akuweke hurum,tangu sasa, kumbuka neno la Mungu linasema"Msipo samehe wengine,nanyi hamtasamehewa na Baba yangu wa Mbinguni" Jiachilie kwa Bwana upate pumziko.

Uliyeteswa na wachawi,mazimwi,mikosi na laana za mababu,njoo kwa Yesu uwekwe huru leo.Kwa Jina la Yesu, uwe mzima; Uondolewe kiu ya umalaya,kiu ya kusengenya,kiu ya ugomvi,kiu ya kulewa,Kwa Jina la Yesu. Ikuachilie. Ujazwe ushuhuda,tunda la roho liwepo kwako tangu sasa. AMEN.
Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

Comments