SABABU ZA KIJANA KUMKUMBUKA MUUMBA WAKE WAKATI WA UJANA

Mwl Abel Suleiman Shiriwa
"Sina budi kuutumia Ujana wangu, kumtumkia Mungu, kwa sababu Hizi zifuatazo"
(1) Mawazo mabaya ya moyo huanza wakati wa Ujana.
Mwanzo 8:21 BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, "Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya Mtu huwa ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.
Muhubiri 11:9 Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako.
Lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.


(2) "Nina nguvu"
1Yohana 2:14 Nimewaandikia ninyi kina Baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo.
Nawaandikia ninyi vijana kwa sababu mna nguvu na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule Muovu.
Kwa hivyo kwa kuwa nina nguvu, basi ni lazima nitumie nguvu za ujana wangu kumtumikia Mungu.

Muhubiri 12:1 Mkumbuke Muumba wako siku za Ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala haijakaribia miaka utakayosema, "Mimi sina furaha katika hiyo"
(3) "Nisipomtukia Mungu katika Ujana ambao ninaweza kujiongoza mwenyewe, sitoweza kufanya hivyo Uzeeni."
Yohana 21:18 Akasema, "Amin, amin, nakuambia; wakati ulipokuwa kijana ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyoosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka."
Kwa hivyo ni lazima nizikimbie Tamaa za Ujana.
2Timotheo 2:22 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ufuate haki na Imani, na upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Katika kuyafanya hayo, ni lazima, nisiruhusu kudharauliwa.
1Timotheo 4:12 Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwa waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na Imani na usafi.
NITAYAWEZA YOTE HAYO, KWA KULIHADHI NENO LA MUNGU.
Zaburi. 119 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii akilifuata Neno lako.
Zaburi 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisikutende dhambi.

MUNGU awabariki sana
By Mwl
Abel Suleiman Shiriwa

Comments