SI KWELI KWAMBA KILA ANAYEPATA SHIDA YA KUSAMEHE ANA ROHO MCHAFU AU PEPO

SI KWELI KWAMBA KILA ANAYEPATA SHIDA YA KUSAMEHE ANA ROHO MCHAFU AU PEPO. Kusamehe ni moja ya mambo muhimu tunatakiwa kuyafanya. You must walk into people's shoes ili kuweza kumsaidia mtu anayesumbuliwa na UCHUNGU unaomfanya ashindwe kusamehe kwa haraka. Wapo watu wengi sana wanatamani sana waweze kusamehe na sio kwamba eti wana roho chafu, hapana. Ni uchungu usioelezeka. Yapo maumivu ambayo huwa ni makali saana sana kiasi kwamba mpaka Mungu mwenyewe akusaidie kupitia Roho mtakatifu ndipo unaweza kusamehe bila kuendelea kusikia uchungu kila ukikukbuka. Watu ambao hawajawahi kuumizwa vizuri kama mfano wa ndugu zetu wa Congo, Rwanda, Burundi, n.k. ambao baadhi yao walivamiwa na watu wabaya, waka-lazimishwa kuwa-twanga watoto wao wachanga kwenye kinu, na wengine wakalazimishwa kuangalia namna wake zao wanafanyiwa unyama, hawawezi kuelewa ugumu wa kusamehe haraka-haraka. Sasa, I don't care how much wewe unalijua neno, it is very important kujua namna ya kusema when it comes to this issue of forgiving others. NI LAZIMA TUWEZE KUSAMEHE IKIWA TUNATAKA TUSAMEHEWE PIA NA TUWEZE KWENDA MBINGUNI INGAWA WAKATI MWINGINE INACHUKUA MUDA NA INACHUKUA PROCESS ILI KUWEZA KUSAMEHE. Yapo mambo rahisi sana ambayo unaweza kusamehe in seconds KUTEGEMEANA NA UMEKUA KIROHO

by
Pastor-Donis  Nkone

Comments