Hayo
yalikuwa maneno ya mlemavu mmoja aliyepanda jukwaani pamoja na familia
yake na wakati mimi nilipokuwa ninaendelea kuhubiri.
Ujumbe wangu niliokuwa nikiuhubiri ulikuwa juu ya nguvu za Mungu ya
kuokoa ,kuponya na kujaza Roho Mtakatifu. Wakati nakaribia nusu ya
ujumbe niliokuwa nauhubiri ,ghafla nilimwona kijana wa kihindi na
familia yake ,taratibu wakitembea kwenye
njia iliyo katikati ya viti wakija jukwaani. Mume alikuwa anachechemea
Sana. Niliwaza “Bwana, hii ni ajabu wanakuja kutoa maisha yao kwako”
Hawakusita walikuja mpaka kwenye madhabahu.Hakuna aliyewazuia wakati
wanapanda ngazi hadi waliposimama mbele yangu.Nilipigwa butwaa nikaacha
kuhubiri na kusema, Niwasaidie nini?
Mtu yule alinitazama kwa
macho makavu na kusema “Umekuwa ukituambia kuwa Yesu yu hai, leo mimi
nina miaka Ishirini na nane na ni kilema,mke wangu naye ana kansa.
Tazama
ngozi ya binti yangu inatoka damu kwa sababu ya ugonjwa na ukurutu
mkali,hakuna mtu aliyeweza kumsaidia.Unasema kuwa Yesu wako anaponya
thibitisha sasa!
Kusanyiko lote lilifunikwa na ukimya wa
ajabu, watu wote walinikazia macho pale jukwaani.Niliwatazama watumishi,
nao walikuwa wameduwaa maana hawakutegemea jambo kama lile kutokea.
Niliwaita kwangu wale watu na kusema, Ndugu zangu tupige magoti na
kumwita Bwana,Kisha nikaomba,”Bwana Yesu mtu huyu ananiambia
nithibitishe kile ninachohubiri ,lakini Bwana mimi sihubiri injili
yangu,nahubiri injili yako wewe,wewe ndio uthibitisho.”Japo kuwa
niliomba kwa ujasiri sikujua nini cha kufanya baada ya hapo.Ilionekana
kama muda nao umesimama,mkutano mzima hakuna sauti liyosikika.Nikiwa
nimepiga goti tu pale huku macho yangu nikiwa nimeyafunga na nikiendelea
kuomba.
Ghafla kukawa na kelele kubwa ambayo ilinishtua
nikaamua kufungua macho,Nilipo angaza macho nilimwona yule mtu,mke wake
na binti wote wamedondoka pale sakafuni na uwepo wa Mungu wa tofauti
ulikuwa umelifunika lile eneo.Baada ya mda mfupi hatimaye walianza
kuinuka,baba alipomtazama binti yake alianza kupiga kelele na kulia huku
machozi yakimtoka.Mikono ya binti yake ilikuwa haitoi damu
tena.Nilishangaa kuona si damu tu iliyokoma bali hata ngozi yake
ilionekana kuwa kama mpya.Muda ule ule baba yake alianza kukimbia
kuzunguka jukwaa,akisema,nimepona nimepona.Mguu wake wenye ulemavu
ulipona dakika hile hile.Mke wake alipoanza kujichunguza naye akagundua
kuwa Mungu amemgusa pia. Uwepo wa Roho Mtakatifu ulibadilisha
mkutano ule kiasi kwamba maelfu ya watu waliamua kusalimisha maisha yao
kwa Yesu siku ile.Roho Mtakatifu anapokuwa kazini ,hatuitaji kuonyesha
au kuthibitisha chochote,Yeye hututumia sisi katika huduma lakini ni
uweza wake na ujumbe wake ndio unaoleta uzima.
Habari hii imenukuliwa na Masawe Gilbert(hapa )toka kwa Mtumishi Benny Hinn Katika kitabu chake”Welcome Holy Spirit”(Karibu Roho Mtakatifu) Ukurasa wa 172-173
Comments