USINGIZI WA KIROHO * sehemu ya pili *

 Na Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Tunapokuwa tumelala kiroho,
kuna hali ya kubadilishiwa jambo jema kwa jambo baya katika ulimwengu wa roho.
Upo mbadilisho/Exchange wa nguvu za kimapepo (Demonic change) ambao hufanyika kwa mtu aliyelala kiroho.Adui ni muongo siku zote maana yeye hana kilicho chema sababu chake kilishakufa,

hata yeye mwenyewe ni marehemu shetani,alishashughulikiwa pale msalabani,Hivyo hana jipya,kazi aliyobakia kwake ni kutafuta yaliyo hai kutoka kwako na kukupa yaliyokufa.

Na katika sehemu ya kwanza nilikupa mfano wa andiko moja, tulikuwa tukijifunza kuhusu habari za wanawake wawili ambao ni makahaba.
1Wafalme 3:16-21.

• Katika andiko hilo tunajifunza jambo moja la msingi ambalo ndio hali halisi itokeavyo katika maisha ya kila siku.

Tunaona mama wa yule mtoto aliyekufa akimdanganya mwenzake mwenye mtoto aliye hai kwamba mtoto wake ndie aliye hai,kwa kumbadilisha nyakati za usiku walipokuwa wamelala.

Adui hutulazimisha kukubali mazingira aliyoyatengeneza yeye kwa UONGO.
Leo ninakuandikia ujumbe huu ili kuweza kukataa taharifa mbaya za ADUI zilizobadilisha Ndoa yako,
Maendeleo yako,
Uchumi wako,
Afya yako N.K

-Leo tunaendelea katika andiko hilo hilo,
Tunasoma;

1 Wafalme 3 :21
“ Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.”

Ukisoma katika Biblia ya kiingereza ya New King James Version (NKJV),utaona andiko hilo limeandikwa hivi;

"And when I rose in the morning to nurse my son, there he was, dead. BUT WHEN I HAD EXAMINED HIM IN THE MORNING,INDEED,he was not my son whom I had borne." 1 King 3:21

Biblia inatuambia kwamba,ilipofika asubuhi akamuangalia sana,alimuangalia mwanaye kwa umakini,/ BUT WHEN SHE HAD EXAMINED HIM IN THE MORNING,INDEED.

*Asing’eweza kumtambua mwanaye pasipo kumuangalia mwanaye kwa ukaribu katika nyakati za asubuhi.

*Haikuwa rahisi kumtambua mtoto wake aliyebadilishiwa pasipo kumtizama kwa karibu/Examining him indeed

*Uonapo biashara yako,Masomo yako,Ndoa yako,Uchumi wako,umekufa gafla,
yakupasa uitizame kwa umakini,
kwa ukaribu,ndipo utagundua chanzo cha cha kifo hicho,
ni kwamba upo mbadilishano wa nguvu za kiroho,/Spiritual exchange,
Sababu chochote ukionacho katika ulimwengu wa mwili kilianzia katika ulimwengu wa roho.

*Mwanamke aliyebadilishiwa mwanaye, alipomuangalia kwa karibu ile kwa sana,ndipo alipogundua kwamba siye mtoto wake,akasema
“ NO! I WANT MY BABY BACK,I WANT MY BABY BACK! I WANT MY BABY BACK !”

*Imefika wakati sasa tusema NO!,NO!,NO! kwa mambo tuliyobadilishiwa na shetani,

*Ipo nguvu ya kukiri,

*Wapo watu ambao wapatapo magojwa,utawasikia wakikubali ile hali na kuiona ndivyo ilivyo,wengi utawasikia.

“Aah! Huu ndio ugonjwa wangu bwana!!”
Watu wa namna hii wamesahau kwamba walipokuwa wamelala kiroho shetani alikuja akapanda magonjwa ndani yao,
maana si Mungu kwa sababu Mungu hutuwazia mawazo ya amani Yeremia 29:11,Bali shetani kazi yake ni kuiba na kuchinja na kuharibu; (Yohana 10:10)

*Hivyo basi,
KULALA KIROHO
*Ni ile hali ya kujisahau kufanya mazoezi ya UTAUWA( hali ya kujisahau kukaa katika uwepo wa Bwana.)…

ITAENDELEA…
*Usikose fundisho lijalo,nitakapomaliza nitafanya maombi rasmi kwako ikiwa utahitaji,mawasiliano 0655-111149.

UBARIKIWE…
Mtumishi Gasper Madumla


Comments