USINGIZI WA KIROHO.*sehemu ya kwanza*

Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Kuna mambo mengi sana yanatokea tunapokuwa tumelala kiroho.Adui huamka tunapokuwa tumelala.
Dhumuni la adui ni kuharibu,
kwa kuiba kile tulichopewa na Bwana Mungu,maana kile tulichopewa na Mungu ni kitu chema sana

*Hivyo kunam-badilishano usio wa halali tunapokuwa tumelala kiroho.Ubadilishano huu ni wa kutumia nguvu za giza/nguvu za kimapepo(A demonic change)

*Wakristo wengi leo wamebadilishiwa vitu au mambo yao ya thamani walipokuwa wamelala pasipo kujijua.Siku ya leo nataka uyajue haya,na tunaanzia kwa andiko hili;

Tunasoma 1 Wafalme 3:19-20;
“ Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia.
Akaondoka kati ya usiku,
akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu.”

*Katika andiko hilo, tunaona habari za wanawake wawili makahaba. Ambao walikuwa wakiishi nyumba moja.Wote wawili wakafanikiwa kuzaa watoto,baada ya kuzaa,mmoja wapo alimlalia mtoto hata kufa nyakati za USIKU.

Biblia inatuambia wakati wa usiku ndipo pakatokea UBADILISHANO/EXCHANGE baina ya mtoto aliyekufa kwa mtoto asiyekufa(1 Wafalme 3:20)

• Mbadilishano/exchange huo ulitokea nyakati za usiku wakati mama wa mtoto asiyekufa alipobadishiwa mtoto wake na kupewa mtoto aliyekufa.

Hivi ndivyo adui afanyavyo wakati tunapokuwa tumelala,
-anajaribu kukuchukulia mtoto wako aliye hai na kukupa aliyekufa,
-anajaribu kukubadilishia Ndoa yako aliyo hai,na kukupa iliyokufa,
-anajaribu kukubadilishia kazi yako nzuri na kukupa mbaya,
-anajaribu kuondoa kizazi kilichowekwa na Mungu ndani yako,na kukupa UTASA.N.K

• Adui ni muongo siku zote,akitaka ukubaliane naye kirahisi kwa kukubadilishia kitu kizuri kwa kitu kibaya.

*Mungu hajakupatia kitu kinyonge,
*Mungu hajakupatia Ndoa yenye matatizo,
*Mungu hajakupatia kazi yenye misukosuko,
*Mungu hajakupatia afya ya magonjwa,
*Mungu hajakupatia kuishi katika umasikini,BALI ADUI NDIYE ALIKUBADILISHIA NYAKATI ZA USIKU ULIPOKUWA UMELALA USINGIZI WA KIROHO.

Haleluya…
Jina la Bwana lisifiwe…

Tazama andiko hilo vizuri (1 Wafalme 3:16-20),
utagundua kwamba haikuwa rahisi kwa mama yule aliyebadilishiwa mtoto wake,maana watoto wote walikuwa ni wachanga mno.

Hivyo adui akapata mwanya wa kutaka kumlazimisha yule mama akubali kumchukua mtoto ambaye si wake,ambaye ni maiti.

Na ndivyo Adui afanyavyo kwetu sisi tunapokuwa tumelala katika usingizi wa kiroho,yeye adui hutulazimisha kukubaliana naye kwa mazingira aliyoyaandaa yeye,akijua kwamba itakuwa si rahisi sisi kugundua.

Sasa angalia;
1 Wafalme 3 :21
“ Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.”
Neno linaposema,

“Nilipoondoka asubuhi…” Hapa maana yake ni kwamba ASUBUHI ni mahali ambapo pana MWANGA wa kutosha,ambao ulimfanya yule mama aliyebadilishiwa mtoto wake kumtambua kwa haraka alipomtizama sana.

Sasa Bwana Yesu Kristo ndiye asubuhi yetu,Yeye Yesu Kristo ndiye MWANGA wetu unaotupa kutambua UBADILISHAONO HUO ULIOFANYIKA USIKU.

Kwa maana nyingine ni kwamba yule mama aliyebadilishiwa mtoto wake,hasingeweza kumtambua mtoto wake nyakati za USIKU,
Hivyo alihitaji mwanga ili aweze kumtizama vizuri mtoto wake,kisha amtambue.

Vivyo hivyo sisi wenyewe hatuna UWEZO wa kutambua mambo yetu yaliyobadilishwa katika ulimwengu wa roho pasipo kuwepo NURU,ambayo hiyo NURU ndiye Yesu Kristo.

*Ninaomba usikose fundisho hili,Maana nitakapomalizia nitafanya maombezi kwako
Mawasiliano yangu ni 0655-111149

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments