Viumbe na Maumbile ya Kichawi



Katika dunia tunayoishi imegawanyika katika sehemu mbili, yaani Ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili. Ulimwengu wa mwili ni ulimwengu ambao unaonekana kwa macho ya nyama. Ulimwengu wa roho, wenyewe una tabia tofauti,
i) ni ulimwengu usioonekana kwa macho ya kawaida.
ii) vitu vyote vilivyoko humo ni roho.
iii) kuna viumbe mbalimbali vya rohoni.

Leo tunaangalia kuhusu Viumbe vya Rohoni. Tukirudi katika Biblia, tunaona kwa habari ya wamisri na vyura, (kutoka 8:2-7) katika mstari wa saba, tunagundua kuwa na waganga nao walifanya vilevile kwa kuleta vyura duniani kama Musa alivyofanya. Kumbe, hata wachawi wanaweza kutengeneza viumbe mbalimbali vya rohoni na kuvidhihirisha katika ulimwengu wa mwili.

Mambo ya Walawi 13:11, hapa tunaona baadhi ya ndege ambao Mungu alikataza kuwa wasiliwe. Utajiuliza kwanini? Jibu ni kuwa kwa kipindi cha agano la kale Yesu alikuwa hajafa bado, hivyo hakukuwa na damu ya utakaso kwa wanyama hao. Mungu alikuwa anatumia njia hiyo ya sheria kuwaokoa wana wa Israeli wasijinajisi na wanyama hao. Kumbe viumbe vya kichawi vilikuwepo tangu agano la kale.

Ndio maana Ayubu 41:1, Luka 10:19, Ufunuo 6:4, Ayubu 39:9, biblia inatumia wanyama kwasababu, Mungu anataka tujue uwepo wa viumbe hivyo vya kichawi katika ulimwengu wa roho. Hivi vyote ni viumbe vya rohoni vinavyotenda kazi dhidi ya maisha ya watu.

Kama vile malaika walivyovaa mwili na kuja kuiangamiza Sodoma na Gomora, vilevile na mapepo wachafu nao huvaa maumbo mbalimbali. Ufufuo 12:7, shetani naye anaweza kujibadili maumbo ya namna mbali mbali ili kuangamiza maisha ya watu. Ndio maana unaweza ukapita mahali, ukasikia kifuu cha nazi kimekusemesha, kwa hakika kile sio kifuu bali ni pepo amejigeuza na kuwa kifuu cha nazi. Mashetani wana tabia za kujibadili maumbo ya aina mbalimbali.

Ni muhimu kuomba kabla ya kutumia vitu ambavyo ama unapewa na mtu, 1Wakorintho 10:31. "31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu." Kumbe kila jambo unalotenda au kabla ya kununua au kuuza unatakiwa ufanye kwa utukufu wa Mung-Pastor Josephat Gwajima

Comments