WATU WA MILKI YA MUNGU* sehemu ya mwisho*

Mtumishi Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiwe…
Watu wanao milikiwa na Mungu hutambuliwa kwa chapa ya Roho mtakatifu,maana hapo mwanzo kabla ya chapa ya Roho wa Bwana walikuwa hawatambuliki,
Yaani tulikuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; tulikuwa hatukupata rehema, bali sasa tumepata rehema .( 1 Petro 2:10)

Hivyo,“Watu wa milki ya Mungu” ni ule uzao mteule,ukuhani wa kifalme,kwa msemo huo tumefananishwa na watoto wa mfalme,mfalme wetu ambaye ndie Baba wa mbinguni.
*Tabia mojawapo ya watoto wa kifalme ni hii kwanza ni kuishi katika mazingira ya kutonyanyaswa au kunyanyasika kwa habari ya maadui.Sababu Adui hana nafasi ya kumuonea mtoto wa mfalme.
Watoto wa kifalme hulindwa muda wote,kwamba wasije kuvamiwa na adui pindi ajapo .

Haleluya…
*Wakristo tumefanyika watu wa milki ya Mungu ili tuitangaze habari njema na wala sio kwenda mbinguni tu,
maana kama kuokoka ni kwenda mbinguni tu basi ni dhahili kabisa tusing’ekuwa tunaishi mpaka hivi leo kwa sisi tuliokoka.

Bali tumefanywa watu wa Mungu kwa madhumuni muhimu kabisa ,kwamba tukaitang’aze fadhili za Bwana Mungu kwa mataifa yote.
Tunasoma 1 Petro 2 :9 ;
“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, MPATE KUZITANGAZA FADHILI ZAKE YEYE ALIYEWAITA mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;”

*Swali la kukuuliza wewe mpendwa uliyeitwa kisha ukafanyika mtu wa milki ya Mungu,kwamba Je umechukua hatau gani pale unapoona baba,mama,au ndugu yako akipotea katika ulevi,uhuni,ukahaba,matusi,na mambo kama hayo?
Kumbuka,tumeitwa ili kuzitang’aze fadhili zake Bwana yaani kupeleka habari njema kwa watu wote haijalishi ni kwa baba yako ,
au mama yako ,
au ndugu zako,
kwamba watakuonaje,wewe mtu wa milki ya Mungu yakupasa kuomba Roho mtakatifu akutangulie ili kuwakomboa watu wa taifa lako.

Ooh,ninampenda Nehemia pale aliposimama kuwaombea ndugu zake waliopo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu.
Nehemia 1 :4;
“ Hata ikawa niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadha wa kadha; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni;”

Lakini hata baada ya maombi hayo ,Nehemia aliona bado haitoshi,kwamba inahitajika aende kuwaona ndugu zake walio katika dhiki nyingi na mashutumu.Huu ni mfano wa kuigwa
Watu wa milki ya Mungu wa siku za leo,wengi wao hawana muda kwenda kuwatembelea ndugu zao wale walio wa kidunia ambao wanaishi katika dhiki nyingi na mashutumu,
wakijiona ya kuwa haiwapasi kwenda na kuwa kati yao.

*Endapo tutashindwa kwenda kuwaona ndugu zetu wasio-okoka kwa kuwapelekea neno hata misaada,tutakuwa hatuko salama kwa wokovu wetu.
MWISHO.
UBARIKIWE.

Comments