WATU WA MILKI YA MUNGU*sehemu ya kwanza*

Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Karibu tujifunze,
Tunasoma 1 Petro 2 :9
“ Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu,WATU WA MILKI YA MUNGU , mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;”

* Biblia inaposema “ Watu wa milki ya Mungu” Ina maana kuwa ni;
-Watu wake Mungu wale muhimu sana “ (His own special people)
ambao ni taifa la Mungu,
wamefanyika sehemu ya Mungu,
yaani ni uzao mteule.

*Sawa sawa na neno la Mungu katika kitabu cha Kumb 4 :20 lisemavyo ;
“Bali Bwana amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuu ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo leo hivi.”

* Ikiwa sisi tu watu wa urithi wake basi sisi ni WATAWALA PAMOJA NAYE.
Na ikiwa ni hivyo basi,neno “MILKI”katika andiko hilo( 1 Petro 2:9)
lina maana ya Uwezo wa kumiliki,
kutawala,Uwezo wa ki-Mungu ulioachiliwa ndani yetu na ndio maana andiko linasema ;

'' WATU WA MILKI YA MUNGU ''
yaani sisi tuna milikiwa na Mungu Baba,hivyo tupo katika sehemu yake ya Uungu na tumefanyika taifa takatifu kama Yeye alivyo mtakatifu. Hapo sasa tunapewa uwezo wa kutawala Labda nikupe mfano kidogo ;

* Tazama mtoto wako awapo nyumbani,anakuwa na uhuru wa kuongea na wewe,au kutembea katika nyumba yako popote pale (Isipokuwa chumbani mwako) pasipo kukatazwa au hata kuulizwa na mtu mwingine.Maana aweza kuenda kibaraz
ani au jikoni au sebureni au kutembelea bustani,N.K

*Kwa mfano huu inaonesha mtoto ana uhuru na uwezo wa kutawala baadhi ya mambo ya nyumbani,
Alikadfhalika Watu wa milki ya Mungu wana uhuru mbali na dhambi,

tena wamepewa uwezo wa kutawala tazama hata pale Bwana Mungu alipomwambia Adamu na Hawa ;
“ Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; MKATAWALE samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Mwanzo 1
:28

• Andiko linaposema sisi ni uzao mteule ina maana kuwa ,Ni watu wenye uzao ndani yetu ambao uzao huo umetokana na Roho (Roho wa Mungu) “ Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. “ Yoh 3 :6 Ikielezea wale waliozaliwa mara ya pili tu, yaani waliookoka.

• Tunaitwa ni uzao mteule maana hatukuokoka kwa akili zetu bali ni kwa kuteuliwa ,tena ni kwa neema tu. Haitupasi kujisifu kwamba, tulikuwa na akili nyingi ndio maana tumeokoka (Waefeso 2 :8)

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments