WATU WA MILKI YA MUNGU*sehemu ya pili*

Mtumishi Gasper Madumla

“ Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, WATU WA MILKI YA MUNGU , mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ” 1 Petro 2:9

Bwana Yesu asifiwe…

Karibu tuendelee,
…Hivyo kumbe Bwana ametuheshimisha mno hata kutuita kwamba sisi ni watu wa nyumbani kwake,
watu ambao ni ukuhani wa kifalme.

Biblia inasema kuwa sisi ni UZAO MTEULE maana yake tumezaliwa kwa Roho kwa sababu Roho wa Mungu yeye anazaa watu wake kuanzia hapo awali mpaka sasa anaendelea kuzaa.

Sisi tuliozaliwa mara ya pili,tunaitwa ni uzao mteule.Nasi yatupasa na sisi KUZAA kuendeleza mzao,
kwa maana Yeye aliyetuzaa ni Roho naye huyo Roho akaa ndani yetu basi tunapozaa,
Ukweli ni kwamba sio sisi tuzaao bali ni Roho ndie azaae,Kumbe jukumu la kuzaa ni letu sote sisi tuliozaliwa kwa Roho Mtakatifu
.
*Yeye azaae atasafishwa ili azidi kuzaa tena,yaani yeye atakaye mleta mtu kwa Kristo atabarikiwa mara dufu.
Tunasoma Yoh 15:2;
“ Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.”

Sisi tukiwa taifa takatifu kama andiko lisemavyo “ Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu,….” (1 Petro 2:9).
Hapo tuna fananishwa na MALANGO katika familia zetu,Koo zetu,Kabila zetu,Nchi yetu.N.K

Tumekuwa wateule ,
watu wa Mungu tukiwa na UTIISHO wa kutamka na ikawa kwa njia ya msaada wa Roho mtakatifu katika jina la Yesu Kristo.
Bwana Mungu anatutizamia tuishi maisha ya ushindi muda wote kwa sababu sisi tu wateule,watu wa Mungu.

Ninafahamu kuwa majumbani tunapoishi ,tunaishi na watu wa namna tofauti tofauti,
Lakini inatubidi tuweze kutofautishwa kati ya watu wa mataifa na watu wa milki ya Mungu,pasipo hata kuanza kujitambulisha,

Yaani watu wenyewe wanapoyatazama matendo yetu wajue hawa hakika ni miungu midogo,watu wa milki ya Mungu,
Na kwamba tunaye Baba.

Ile namna ya kuwa na Baba Mungu maishani mwetu, inatupelekea kutoonewa onewa na ibilisi pamoja na mapepo yake,

Ngoja nikupe mfano kidogo;
*Mimi nakumbuka nilipokuwa mdogo,mtu yeyote akinichokoza tu,ni lazima nikamsemee kwa baba yangu,
yaani akiniudhi tu gafla utanikuta nishafika kwa baba namsemea maana niliamini kuwa baba yangu anao uwezo wa kuwapiga watu wote

,sababu alikuwa akinipiga mimi,hivyo nikajua atakuwa anawapiga watu wote,tena nikifika kwa baba ninapata Amani na kumueleza kwa furaha kwa sababu tumaini langu lilikuwa kwake.

*Alikadhalika sasa,sisi ambao ni watu tuliooshwa kwa Damu ya mwana kondoo ,hatuko yatima tunaye Baba ambaye mwenye uwezo mkuu kuliko yeyote Yule aliyekuweko,aliyeko,wala atakayekuja.

*Hivyo hatuna haja ya kulia lia muda wote tunapopitia majaribu,au ibilisi ajapo kukujaribu wewe.
*Ikiwa shetani ajapokuja kwako,usilie lie, bali kumkabidhi huyo shetani/jaribu kwa Bwana Yesu kisha uone kama hatakimbia mwenyewe.

*Kulia lia ninakokuzungumzia hapa,ni kule kuwa tayari kuwanyenyekea watu wa miungu kwa sababu eti wewe unashida Fulani NO! nasema Yupo Mungu hajakuacha bado maana ukimuita huja.

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments