Wokovu Ni Kwa Wote


katika mazingira ya vita mwanajeshi akibatizwa ma mwanajeshi mwenzake ambaye ni mtumishi wa MUNGU  baada ya kumpa YESU maisha yake
 Matendo 10:1-8, 17-48  Wagani ambao MUNGU aliwatuma, walifika nyumbani kwa Petro. Walikuwa Wayunani. Kisha Petro aligundua kwamba MUNGU anataka Petro awaone Wayunani kama anavyo waona Waisraeli. Yaani Wayunani sio watu najisi. Kisha Petro na rafiki zake Waisraeli, pamoja na Wayunani watatu waliondoka. Yopa na walienda mahali palipoitwa Kaisarea. Kisha wakaenda nyumbani kwa Kornelio. Kornelio alikuwa Myunani. Pia alikuwa jemedari wa jeshi la Warumi. Kornelio alikuwa mtu mcha MUNGU. Familia nzima ya Kornelio alikuwa wanampenda MUNGU. Kornelio alifanya mambo mazuri mengi kwa watu wa Israeli. Siku chache zilizopita, MUNGU alimtuma malaika kuongea na Kornelio, " Malaika akasema, Kornelio MUNGU amependezwa na sadaka zako na maombi yako yamekubaliwa na MUNGU". Sasa uwatume watu waende Yopa. Na wamtafute mtu anayeitwa Petro na wamwalike aje akutembelee. Wakati huo ndipo Kornelio alipo watuma watu waende Yopa. Petro na rafiki zake wakafika nyumbani kwa Kornelio. Na walipoingia ndani Kornelio akapiga magoti mbele ya Petro (ili kumheshimu). Lakini Petro akasema, "Hapana usimame! Mimi sio MUNGU, mimi ni mtu tu" Kisha Petro akaongea na watu ambao walikuwa ni Wayunani waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa Kornelio. Petro akasema, " Enyi Wayunani manajua kwamba ni kinyume cha sheria ya Waisraeli kwa mwisraeli kama mimi kuingia katika nyumba ya Wayunani. Lakini MUNGU alinionyesha katika maono. Kwamba nisiwaone Wayunani kama watu najisi. Kwahivyo nimekuja kwenu. Kornelio akamwambia jinsi malaika wa MUNGU alivyoongea naye. Kisha Petro alimwambia Kornelio habari za Yesu. Kornelio na familia yake wakamwamini YESU KRISTO na kupokea ROHO MTAKATIFU. MUNGU akubariki sana na kumbuka kuwa MUNGU anawapenda watu wote, haijalishi lugha, kabila au rangi za ngozi. Anataka watu wote wamwamini YESU KRISTO na wamtumikie.
WAKRISTO WAKIWA KANISANI DPC DAR ES SALAAM
ubatizo

Comments