ANDAA MOYO WAKO ILI JAWABU LAKO LITOKE KWA BWANA.*sehemu ya tatu*

Na mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe..
Karibu tuendelee pale tulipokuwa tumeishia katika sehemu ya pili;
Karibu;

...Kanuni mojawapo ya KI-MUNGU ya kupokea kwa kile unachokiomba ni kufanya maandalizi ya kutosha ya roho yako.

01.TOBA
*Mungu hapendi mtu yeyote apotee bali afikilie toba,kwa maana palipo na TOBA pana urejesho wa Roho mtakatifu ambaye kwa huyo Mungu huweza kuachilia jawabu.(Luka 15:1-7) pia
2 Petro 3:9

*Urejesho wa Roho mtakatifu hutufanya tuweze kuzungumza na Mungu moja kwa moja.

Mfano;
-ADAMU kabla ya anguko la dhambi ,yeye Adamu alikuwa akiwasiliana na BWANA MUNGU moja kwa moja,wakati wa jua kupunga,
tazama
Lakini dhambi ilipotokea tu,gafla Roho mtakatifu naye akaondoka ndani ya roho ya Adamu,
na kufanya Mungu kushindwa kumuona Adamu mahali pale alipotakiwa kuwapo,

Tunasoma
Mwanzo 3:9;
“ Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?”

• Hivyo leo tunapotaka kuandaa roho zetu yatupasa kufikilia TOBA kwanza
Tazama Petro naye alijua siri hii Petro akiwaambia watu waliochomwa mioyo yao baada ya kusikia neno la Mungu,
tunasoma
Matendo 2:37-38

“ Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”

Nasema hivi Petro alijua siri ya kuandaa moyo wa mwanadamu,na ndio maana anaanza kwa kuwaambia TUBUNI.
• Kitendo cha kutubu ni cha mwanadamu mwenyewe.

KUTUBU;
-Ni kujisalimisha mbele za Baba wa Mbinguni kwa kuzingatia moyoni kugeuka na kuacha dhambi kwa msaada wa roho mtakatifu.

-Ni kuomba msamaha kwa kujutia dhambi zote kwa zile ulizozifanya,tena kwa zile unazozikumbuka,na hata zile usizozikumbuka,tena kwa zile unazozijua na hata zile usizozijua.

*Kwamba Mungu akusamehe ili uanze moja na Yeye Mungu,upate ondoleo la dhambi,urejee kwake.Kisha tuweze kupokea kipawa cha Roho mtakatifu ambayo ni ahadi yetu sisi sote.

*Kumbuka;
Mungu wetu ni mtakatifu ,
kupita maelezo yoyote yale yaliyopo Duniani,hivyo hawezi kuachilia jawabu lake kupitia ulimi wako wenye dhambi kwa kile unachokiomba kiwe.

Nimesema TOBA ni kuzingatia moyoni kuacha na kuchukia dhambi kwa uweza wa Roho mtakatifu.

*Ni kweli kwamba ;
Hakuna mwanadamu ambaye anaweza kuacha dhambi kwa kutumia akili na ufahamu wake binafsi.
Bali tunao uwezo wa kuacha dhambi kwa msaada wa Roho mtakatifu peke yake kwanza kwa kuzingatia mioyoni mwetu kuzichukia dhambi.
Napenda mfano wa mwanampotevu Biblia inasema ;

Luka15:17-18
“ ALIPOZINGATIA MOYONI MWAKE, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako;”

Kumbe!
*Swala sio kutubu kama kutubu tu,bali swala ni kuzingatia moyoni katika toba.

-Yaani kugeuka moja kwa moja kotoka moyoni katika uasi.
Kuzingatia maana yake ni kutia mkazo kwa kugeuka kabisa.

Tazama mfano huo wa mwana mpotevu,
pale alipozingatia moyoni mwake wala hakurudi nyuma tena bali aliondoka na kwenda kwa Baba yake.

• Labda nikuulize kwamba,Leo hii ni mara ngapi unasema unataka kuiacha dhambi fulani na unaomba Roho mtakatifu akusaidie lakini unajikuta bado ukifanya dhambi ile ile ?

Yaani kama vile kama hukuomba TOBA.Ikiwa hali iko hivyo,basi ni dhahili kabisi kuna tatizo sehemu fulani.
Tatizo hilo si jingine bali ni KUSHINDWA KUZINGATIA MOYONI KWA KUAMUA KUGEUKA KUTOKA KATIKA DHAMBI.

*Nakuambia leo,hata kama utamuomba Roho mtakatifu akusaidie ni kweli atakusaidia lakini msaada huo hautakuwa na maana kama ukishindwa kuzingatia moyoni juu ya toba hiyo uifanyayo.

*Kupitia toba halisi kunakuachiliwa mbali na vifungo vya dhambi
Zaburi 103:3
“ Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,”

Panapo na dhambi magonjwa hayakosi
Kwa sababu magonjwa ni dalili ya uwepo wa dhambi.

Note.
*Sisemi kwamba kila mwenye magonjwa ametenda dhambi,la hasha!
Kwa maana wapo wengine wenye kupitishwa katika majaribu kwa njia ya magonjwa,
Mfano Ayubu mtumishi wa Mungu aliye mkamilifu.Yeye Ayubu hakupata magonjwa kwa sababu alimtenda Bwana Dhambi,Bali kwake ilikuwa kama mtihani (Soma Ayubu 2:6-7)

*Hivyo mwanadamu anapouandaa moyo wake kwa njia ya toba ,humfanya Bwana Mungu amtazame mtu huyo kwa namna ya tofauti sana.
*Pia kuna kibali kinachoachiliwa na Bwana Mungu pindi urejeapo kwa TOBA,kupitia kibali kuna mpenyo,kuna jawabu la ulimi kutoka kwa Bwana

Mfano ;
Tazama habari za Nehemia pale alipoletewa habari mbaya ya mashutumu na dhiki nyingi ya ndugu zake waliopo huko uhamishoni.
Biblia inatuambia alipopata habari hizo akaomba mbele za Bwana,na AKATUBU KWA AJILI YA NDUGU ZAKE.

Nehemia 1: 6 ;
“ tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako,
ninayoomba mbele zako wakati huu,
mchana na usiku,
kwa ajili ya wana wa Israeli,
watumishi wako; hapo NINAPOZIUNGAMA DHAMBI za wana wa Israeli, tulizozifanya juu yako; naam, mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.”

Sikia;
Baada ya mombi hayo ya Nehemia ,
Sasa Mungu anamtaharakisha mfalme Artashata kumpa kibali cha kwenda kuwatizama ndugu zake,

na tena Nehemia akapewa kikosi cha jeshi,na wapanda farasi,Ambapo haikuwa rahisi maana yeye alikuwa hastahili kupata hayo yote kwa sababu yeye alikuwa ni mnyweshaji wa mfalme tu.
Lakini kibali kiliachiliwa baada ya maombi na TOBA.

ITAENDELEA...
UBARIKIWE.

Comments