ANDAA MOYO WAKO ILI JAWABU LAKO LITOKE KWA BWANA *sehemu ya mwisho *

na mtumishi Gasper Madumla


Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…

Ninakukaribisha katika sehemu ya mwisho ya fundisho hili zuri.
Kumbuka mstari wetu tuliokuwa tunasimamia katika fundisho hili ambao ni Mithali 16:1
“Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.”

-Tunaposoma kwamba “ …Bali JAWABU la ulimi hutoka kwa Bwana.” Tuonapo neno “Jawabu” limetajwa,basi ujue lipo swali hapo mwanzo na ndio maana unaona neno JAWABU likitajwa.

*mfano,
magonjwa,
udhaifu .N.K ni baadhi ya maswali kwetu,Lakini Biblia inatuambia JAWABU la Bwana lipo kupitia ulimi wetu.
Hivyo ili Bwana aweze kuachilia jawabu lake kupitia ulimi wetu pindi tuombapo basi ni lazima tufanye maandalizi ya kutosha ya roho zetu.

Kumbuka tulikuwa tukiangalia njia za kufanya maandalizi ya roho zetu,na nikakuambia kwamba njia ya kwanza ni ;
01.Toba
02.Kuandaa sadaka nzuri mbele za Bwana
( Pitia sehemu zilizopita kwa ajili yakujifunza zaidi juu ya njia hizi)

-Na sasa tunaendelea,tulipoishia;
Hivyo basi, kwa habari ya toba hufanya mouvu ya mtu kughailishwa.

*Tunasoma ;
1 Wafalme 21:27-29;
“ Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole.
Neno la Bwana likaja kwa Eliya Mtishbi, kusema,
Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu?
Basi kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake.”

*Biblia inasema kuwa Mungu alighairi uovu aliouandaa juu ya Ahabu ambaye alikuwa ameshiriki dhambi ya mauaji ya Nabothi.(Soma 1 Wafalme 21:1-29)

Mambo mawili ya msingi tunajifunza kupitia andiko hilo ni ;
(i)TOBA hufanya uovu uliokusudiwa kutekelezwa usitekelezwe kabisa,-mfano wa maovu yalighairishwa na Bwana Mungu pale Ahabu alipojidhili mbele za Bwana kwa njia ya TOBA.

Kumbe!
hata kama tuna dhambi za namna gani lakini tukimuendea Bwana Mungu kwa njia ya toba Yeye Mungu yuko tayari kutusamehe.

(ii) YATUPASA KUOMBA KWA AJILI YA WATOTO WETU/AU KIZAZI CHETU.
*Tazama andiko hilo hilo,utagundua kwamba Mungu alimsamehe Ahabu juu ya dhambi yake,
Lakini Bwana Mungu anasema :
“ Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu? Basi kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake.”1 Wafalme 21:29

*Wakristo wengi hatuna tabia ya kuwaombea toba watoto wetu.Na hivyo tukifikiri kuwa Mungu atawasamehe tu pasipo toba yoyote,Kumbe sivyo bali yatupasa kuwaombea toba.
Yatupasa tuige mfano wa Ayubu alipokuwa akiomba toba kwa wanawe kwamba yamkini wamefanya dhambi.( Ayubu 1:5)

• Mungu akusaidie wewe mpendwa msomaji,uwe na moyo wa kuombea TOBA watoto wako,familia,mke/mume wako .N.K

Kumbuka,
Tunajifunza njia za kuandaa roho zetu ili jawabu la Bwana lije kupitia ndimi zetu kwa msaada wa Roho mtakatifu.

*Njia ya tatu ambayo tunaweza kuitumia katika kufanya maandalizi ya roho zetu pindi tunapoomba mbele za Bwana,nayo ni;

03.KUWA NA ROHO ILIYOCHANGAMKA PINDI UMUENDEAPO BWANA.

*Wapo wakristo ambao wanapoenda mbele za Bwana wakati wa ibada,utawaona kama vile wanalazimishwa .Hali hii inazuia bubujiko la ndani,hivyo inakuwa ni vigumu kwa mkristo asiyekuwa na bubujiko la ndani yaani moyo uliochangamka,
apokeeyale ayaombayo.
Kumbuka tunajifunza kuwa
“ Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;.’’Mithali 16:1,Hivyo umepewa jukumu la kuandaa roho yako.

Sikia;
Mchungaji/Mwalimu/mwinjilisti wako ana sehemu ndogo sana katika kuandaa roho yako kwa habari ya maisha ya wokovu.Lakini sehemu kubwa iliyobakia ni yako mwenyewe ukisaidiwa na Roho mtakatifu.

Sasa ikiwa mtu anamuendea Bwana kwa njia ya maombi kisha akiwa na moyo usiochangamka,ninakuambia kwamba itakuwa ni vigumu kwake kupokea vya madhabauni.

*Kumbe yatupasa tuwe na changamko la ndani hata kabla hatujafika kanisani.

Mfano mwamini awapo nyumbani kwake ikiwa anajiandaa kwenda ibadani,basi anapaswa awe na shauku ya kujiandaa kiroho,awe na bubujiko la moyo uliochangamka kwa ajili ya kupokea yale ambayo anatarajia kuzungumza na Bwana Mungu wake.
Hivyo ikiwa ndio wewe sasa ,

Mfano;
-Tazama sasa ,yaani ile usiku wa jumamosi kuamkia jumapili basi,unaanza ku-feel/kuisikia Ibada ikiendelea ndani ya roho yako,hapo MRIPUKO WA AJABU wa kiroho unaanza,
tena ,
tenzi za rohoni zikikutoka,
ukiwa na shauku ya kwenda kuzungumza na Baba wa Mbinguni ibadani hata kama ulikuwa bafuni basi unajikuta tu ukishindwa kujizuia kuimba kwa kusifu na kuabudu,

yaani hata ufikapo ibadani mlipuko wa kusifu na kuabudu katika roho na kweli utaendelea na hali hii inakufanya kupokea kwa urahisi sauti ya Mungu kupitia mtumishi anayehudumu siku hiyo.

Ninakuambia hata mtumishi akihubiri kidogo tu,basi unajikuta unapokea kupita maelezo.Biblia inasema
“ Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa" Mithali 17:22

MWISHO.
UBARIKIWE. Mawasiliano 0655 111149

Comments