ANDAA MOYO WAKO ILI JAWABU LAKO LITOKE KWA BWANA.*sehemu ya nne*

na Mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…

-Ninakukaribisha mpendwa katika fundisho hili zuri sana ambapo tunajifunza jinsi ambayo mwanadamu aweze kuandaa moyo wake ili jawabu la Bwana lipitie katika ulimi wake,
sawa sawa na neno la Mungu kupitia katika Mithali 16:1.

Kumbuka tulikoishia;
Tulikuwa tumeishia katika habari ya TOBA ikiwa kama hatua mojawapo ya kwanza ya kuandaa moyo wako ili Bwana aweze kuachilia jawabu kupitia ulimi wako.(Soma fundisho lililopita ili tuwe pamoja muda huu tunapoendelea)
• Sasa tunaendelea;

Njia ya pili itakayomuwezesha mwanadamu kuandaa moyo wake kusudi apokee jawabu kutoka kwa Bwana pindi aombapo ni;

02.KUANDAA SADAKA NZURI WAKATI WA IBADA.

* Watu wengi hawamtolei Mungu sadaka iliyonona tena cha kushangaza ni kwamba watu hao hao ndio wanaomtaka Bwana aweze kuwatendea miujiza katika yale wanayoyaomba.

-Sadaka iliyonona ni sadaka iliyo nzuri mbele za Bwana,
-Sadaka iliyonona ni sadaka yenye kupendeza machoni pa Bwana,si sadaka kilema.
-Sadaka iliyonona ni sadaka yenyekusukw-sukwa,yenyekujitosheleza,yenye harufu nzuri mithili ya dhabihu ya mwana-kondoo wa kuteketezwa kwa ajili ya Bwana.N.K

• Tunachotafuta hapa ni kwamba ;
Mungu awezekupitisha JAWABU/MAJIBU kwa yale tunayoyaomba,Basi hatuna budi kwanza tuandaye mioyo yetu kwa TOBA pamoja na kubeba sadaka nzuri wakati wa ibada,kwamba ;

*(i) MOYO WA TOBA- uturejeshea uso wa Bwana,ili Bwana Mungu atutizame kwa sura nyingine(soma fundisho lililopita kwa habari ya TOBA kama njia ya kuandaa moyo/roho yako)

*(ii) SADAKA ILIYO NZURI-Humshawishi Mungu kulidhia yale tuyaombayo kwa jina lake,naye huweza kupitisha jawabu.

*Sadaka nzuri huandaliwa kuanzia mwanzo wa wiki,
Mfano;

-kuanzia jumatatu mtu aweza kuandaa sadaka yake,ifikapo siku ya IBADA inakuwa sio suala la kukosa sadaka au inakuwa sio suala la kushtukizwa.

-Watu wengi hawafanyi maandalizi haya,hivyo hujikuta wafikapo siku ya Ibada wanatafuta sadaka yoyote ile waliyokuwa nayo wakati ule,
kama itakuwa ni shilingi mia,
au shilingi mia tanao katika pochi/suruali basi hutoa hiyo hiyo na wakidhani kuwa Mungu atalidhia hiyo sadaka yao.

*Sadaka hiyo ni sadaka KILEMA ambayo Mungu haitaki kabisa! Maana yeye asema ;
“ Tena mtoapo sadaka aliye kipofu,
si vibaya?
Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa,
si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako;
je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema Bwana wa majeshi.” Malaki 1:8

• Sadaka nzuri ndio hukamilisha ibada
-Yaani niseme hivi;
• Ibada pasipo sadaka si ibada.

-Siri hii ,watumishi wa Bwana waliifahamu,na ndio maana hata ukianzia kwa Ibrahimu.

-Pale Mungu alipozungumza naye tu ,utaona Ibrahimu akijenga madhabahu kisha na kutoa Sadaka iliyonona,alikuwa akifanya hivi ili kukamilisha Ibada yake yeye na Mungu,
Alikadhalika hata watu wengine wa Mungu walipotokewa na Bwana utakuta ni lazima watoe SADAKA ILIYO NZURI MACHONI PA BWANA.

*Mitume nao walijua siri hii,tazama Matendo 14:8-14
Katika mstari wa 13 umeandikwa hivi;
“Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng'ombe na taji za maua hata malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano.”

*Ukisoma mstari wa 14,utaona wakina Paulo wakiwakataza kabisa wasijitolee SADAKA maana wanajua pindi watakapotoa tu,watakuwa wamekamilisha ibada yao ya sanamu.

*Ipo siri kubwa sana iliyofichika ndani ya sadaka nzuri,maana kupitia sadaka hiyo nzuri Bwana aweza kughahili uovu wote uliopangwa juu yako.
Tazama habari ya NUHU pale alipomtolea Bwana Sadaka iliyonona baada ya gharika,
tunaona Bwana anaghahili kumuangamiza mwanadamu,
( Mwanzo 8:20-21)

*Hivyo mtu aweza kuandaa moyo wake kwa njia ya sadaka iliyokamilika pindi amuendeapo Bwana…

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments