Askofu Kakobe akanusha uvumi wa kulikimbia Kanisa lake.


Askofu Zakary Kakobe
ASKOFU wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship amekanusha uvumi ulio tapakaa kwa Watanzania yakuwa amewakimbia wakristo wake na kuenda nchi za nje.

Alikanusha uvumi huo baada ya kuongoza mazishi ya aliyekuwa Askofu wa kanisa la Christian Love lililopo  Kiwalani, aliyefaliki tarehe 2 Agosti mwaka huu.

Mazishi ya mchungaji huyo yaliambatana na ibaada ambayo iliongozwa na Kakobe katika makaburi ya Kinondoni juzi. Kakobe alisema kuwa yeye hajaondoka nchini kama Watanzania wengi wanavyosema. 

"Sijaondoka na siwezi kuondoka kwasababu mimi ni wa hapahapa na nitazidi kuwa hapahapa, na tutabanana hapahapa, hakuna kwingine tena. Huwa natoka kihuduma tu na huwa narudi tena, na sio kuwa nimehama", alisema Kakobe

Kumekuwa na ukimya sana kwa Askofu huyo kitu kinachowashangaza wengi, kwani walishazoea kumuona akiongea kwenye vyombo vya habari mara kwa mara.
 
Mmoja wa wakristo wake alikili kuwa kwa sasa Askofu wao amepoteza umaarufu tofauti na zamani ndiyo maana watu wengi wanafikia uamuzi wa kufikiri hayupo nchini.

Kwaupande mwingine kinachoshangaza ni kwamba ujio wake katika msiba huo wa Askofu mwenzake ilikuwa ni safari ya kutokea nchi za nje ambapo aliingia nchini siku ya jumapili ya Agost 4 mwaka huu. 

CHANZO: GOSPEL NEWS MEDIA

Comments