Askofu Dr.Moses Kulola enzi za uhai wake |
Taarifa imetolewa na Mchangaji Daniel Kulola kupitia mtandao wa kijamii wa facebook kuwa mzee wetu Askofu Mkuu wa EAGT askofu MOSES KULOLA amefariki dunia. hii hapa ripoti hiyo
''WATU WA MUNGU SALAAM, NINA SALAAM ZA MAJONZI. BABA YANGU MZEE KULOLA AMEFARIKI... MUDA SIYO MREFU''.
MWANAYE Dr. DANIEL KULOLA
Askofu mkuu na mwanzilishi wa kanisa la EAGT nchini Tanzania Dr.Moses kulola amefariki Dunia jijini Dar es Salaam ambapo alikua akiendelea na matibabu katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.
Askofu .Dr Moses Kulola katika mwaka huu alikua akisumbuliwa na matatizo ya kiafya hali iliyopelekea kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi ambapo hivi karibuni alirudishwa nchini Tanzania kuendelea na matibabu yake mpaka Bwana alipomtwaa akiwa na umri wa miaka 85.
![]() |
ASKOFU MKUU MOSES KULOLA ENZI ZA UHAI WAKE NA HAPA ILIKUA NI VIWANJA VYA JANGWANI MWAKA JANA |
![]() |
Askofu Moses Kulola na Mchungaji Daniel Kulola |
Comments