BAADA YA KUOKOKA, TAFUTA UTAKATIFU


Kuokoka ninako kuzungumzia hapa, ni KUOKOKA kwa kunusulishwa na Jehanamu ya moto wa milele, huko ni kuokoka mwili na roho.
JE, UTAWEZAJE KUOKOKA?
Warumi 10:9-10=Kwasababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni Bwana, nakuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA
Kwamaana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata kupata WOKOVU. 


Mpendwa, kuna watu wamekuwa wakienda makanisani, na mchungaji anaposema wanaopenda KUOKOKA kwa hiali yao watoke mbele ili waweze kuongozwa sala ya toba, na namna ya kumkiri Yesu kwa vinywa vyao, watu wengi hutoka mbele, lakini baada ya kuongozwa sara ya toba, na kumkiri Yesu Kristo yakuwa ni Bwana, na Mwokozi wa Maisha yao, watu hawa wamekuwa wakiendelea na maisha yao ya kawaida tu, wala hawana tena habari ya kuendelea kuishi katika mafundisho ya kuukulia Wokovu, hivyo ni wazi kwamba watu hawa hawana tena haja ya kuutafuta huo utakatifu, furaha yao wao ni kujiita Walokole tu, ila matendo yao yako mbali na Mungu,


nje ya kanisa, watu hawa ni Waongo, Wasengenyaji, Wazinzi, Wana chuki, Wafitini na Wagombanishi, tena ukiwachunguza vizuri utagundua watu hawa ni Wakristo wa Jumapili tu.
Mpendwa, Kwa matendo yako ndipo watu watakutambua kama wewe ni Mwana wa Mungu au wa Ibilisi, kujiita umeokoka na wakati matendo yako hayakutambulishi kama kweli Umeokoka, huko ni kujiongezea mzigo wa dhambi.
MWINJ GERALD ROBERT

Comments

iscaca said…
Mungu awabariki sana kwa huduma mnayoifanya.