BWANA ANA HAJA NAWE * sehemu ya pili *

Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe....
Haleluya...

Karibu mpendwa katika fundisho hili zuri ambalo lina makusudi kabisa kwako wewe mpendwa usomaye ujumbe huu.
Kumbuka tulipoishia katika sehemu iliyopita,kumbuka nalikuambia kwamba "Bwana ana haja nawe"na tulisoma katika kitabu cha Luka 19:29-31.
*Ni habari ya mwana-punda aliyefunguliwa kwa ajili ya kazi ya Bwana kwa sababu Bwana alikuwa ana haja nae.Alikadhalika wewe unaweza ukawa umefungwa eneo fulani,kwamba upo kifungoni umeshindwa kufanya yale yakupasayo kufanya,hivyo umefanana na mwana-punda aliyefungwa
LAKINI LEO lPO NEEMA YA PEKEE,MAANA BWANA ASEMA HIVI SASA ANAWATUMA WATUMISHI WA MUNGU ILI UFUNGULIWE,KWA SABABU ANA HAJA NAWE.

Biblia inasema katika kitabu cha Luka : 31
" Na kama mtu akiwauliza,Mbona mnamfungua?
Semeni hivi,Bwana ana haja naye "

Kumbe !
Wapo watu watakaokuuliza wakati unapomfungua mwanapunda aliyefungwa,yaani ni kweli umetumwa na Bwana ukamfungue huyo aliyefungwa lakini bado wapo watu watakao kuuliza,kwamba;

" Mpona wamfungua ? "

Leo wakati unapoenda kufanya kazi ya Bwana ujue ni lazima utakutana na watu wa namna hii watakao kuuliza
"Vipi mpona wafanya hivi?je ni kweli kwamba waweza kuwafungua waliofungw?N.k "

Ooh Haleluya..
Bwana Yesu atuambia sasa,
Tutakapoulizwa basi tuwaambie kwamba;

" Bwana ana haja nao "

* Watu wa namna hiyo si watu kama watu bali ni roho za yule mwovu zilizokaa ndani ya watu,zinazopingana na kazi ya Bwana iliyopo ndani ya watumishi wa Bwana.

Sikia;
Biblia inatuambia kwanza Bwana alipowatuma wanafunzi wake kwenda kumfungua mwanapunda wapo watu walowauliza,

Neno " Kuuliza " katika ulimwengu w roho huwakilisha " kikwanzo/nguvu ipinganayo na nguvu y Mungu "

Ipo vita katika ulimwengu wa kiroho ipiganayo pindi mtu mmoja afunguliwapo,maana adui hapendi kuona hata mtu mmoja anakwenda ka Bwana Yesu.
Lakini hata iweje katika vita hiyo ya kiroho,shetani hana mamlaka ya kuzuia mwanapunda ambaye Bwana ana haja naye.

Maana shetani ni marehemu tu maana alishapigwa pale msalabani,
hivyo hana uwezo tena kuwazuia wale wenyekuhitanika na Bwana.

Haleluya...

Hakika Bwana ana haja nawe , Yeye Bwana hajakuacha bali wewe ndio uliomuacha Bwana kwa sababu tu yawezekana umefungw,U kifungoni
Lakini nami nakutangazia kwamba muda wa kuachiliwa ndio sasa,muda muda wa kufungwa umekwisha,nasema umekwisha.

Luka 19:35
" Wakampeleka kwa Yesu,wakatandika nguo zao juu ya mwana-punda,wakampandisha Yesu."

Huyo mwanapunda alipelekwa kwa Bwana Yesu,na wale walotumwa kumfungua ni wanafunzi wa Yesu,hapa tunajifunza kitu kikubwa sana,
Kwamba wanafunzi wa Yesu wa leo ni mimi na wewe uliyeokoka na kumpenda Yesu kwa kutembea katika sheria zake.

Sisi tuliokuwa wanafunzi wa Bwana Yesu pindi tunapotumwa kwenda kuwafungua wale wote waliotumwa ni lazima tuwafungue kwa jina lake Yeye aliyetutuma ambaye ni Yesu,ndio maana tunaambiwa kwamba

Iwapo tutaulizwa basi tuwaambie kwamba ni Bwana ndie mwenye haja nao wale waloofungwa.

Lakini tazama kwa makini huo mstari wa 35 (Luka 19 :35)
Utagundua kwamba ;
Wanafunzi wa Yesu walipomfungua tu huyo mwana-punda wakampeleka kwa Yesu moja kwa moja bila hata kupita kona kona.

Walompeleka kwa Bwana Yesu kwa sababu Bwana alikuwa ana haja naye kwa kazi yake Bwana,kwa maana hiyo kama Bwana asingekuwa ana haja naye basi asingewatuma watumishi wake wamfungue.

Kama ilivyo leo,wewe uliye-okoka umeokoka sio ili uende mbinguni tu,la hasha sio madhumuni ya pekee.

Bali umeokoka kwa ajili ya matumizi ya Bwana yaani kwa ajili uyafanye mapenzi yake Bwana.Kwa maana alikookolesha kwa sababu Bwana ana haja nawe.

Hivyo tupo hivi kwa ajili ya Bwana,

* Kwa maombezi na kujuliana hali pia,
Mawasiliano yangu ni 0655 111149

ITAENDELEA...
UBARIKIWE.

Comments