BWANA ANA HAJA NAWE."*sehemu ya kwanza*

Na Mtumishi Gasper Madumla


Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…

Ninachoweza kukuambia siku ya leo ni kwamba “ Bwana ana haja nawe” "The Lord has need of you"
Bwana Yesu anataka akufungue kutoka katika vifungo ulivyofungwa,pia anataka akutumie kwa kazi yake,
Yeye Bwana anakutaka hivyo hivyo ulivyo bila kujali kabila lako,
ukoo wako,
rangi yako,
kimo chako,
taifa lako,
lugha yakoN.K.

Ingawa unaonekana huna thamani machoni pa watu,Lakini ninakuambia leo ,wewe ni wathamani machoni pa Bwana.
Nasema hivi ;
“Bwana ana haja nawe”

Tunasoma 19: 31-34
“ Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji.
Na wale waliotumwa wakaenda wakaona kama alivyowaambia.
Na walipokuwa wakimfungua mwana-punda,
wenyewe waliwaambia, Mbona mnamfungua mwana-punda?
Wakasema, Bwana ana haja naye.”

Bwana Yesu aliwatuma wanafunzi wake waende mpaka katika kijiji kinachowakabili na huko watamuona mwana punda aliyefungwa.

Yesu alichaona kuwa yupo mwana punda ambaye amefungwa,kama ilivyo leo Bwana Yesu ndiye aonaye kabla ya sisi kuona.

Mwanapunda huyu alikuwa amefungwa,
Mwana punda aliyefungwa yupo utumwani,yupo kwa ajili ya kumtumikia Yule aliyemfunga.

Katika fundisho la leo tunamuangalia mwana-punda kama mtu aliyefungwa na ibilisi hata kushindwa kufanya yampasayo kwa ajili ya ufalme wa Mungu.

Mwana-punda aliyefungwa ni mtu asiyekuwa na uhuru,tena ni mtu anayetumika katika ufalme wa giza kwa kujijua au kutojijua.
Yupo mtu mmoja siku ya leo yamkini amefungwa yawezekana ni wewe usomaye ujumbe huu,

*lakini usihofu maana Bwana anasema “ana haja nawe.”

Yeye Bwana amanituma kama wale wanafunzi wawili walivyotumwa kwa mwana punda.nami ninakuambia kwamba “ “BWANA ANA HAJA NAWE”

Kitu kimoja kutoka kwa Bwana anachokihitaji kutoka kwako ni kukufungua kutoka katika vifungo vya mateso kisha akutumie kwa kadri atakavyo Yeye.

Kumbuka kwamba mwana-punda alikuwa amefungwa katika kijiji kilichokuwepo karibu na “ Bethfage” na “Bethania”

Ikimaanisha kuwa mahali ambapo mwanapunda huyo alipokuwa amefungwa ni sehemu ya kimasikini yaani ni sehemu duni ,maana neno “ Bethnia” huwakilisha “ nyumba ya maskini”

*Kiyahudi neno “BETH=nyumba,NIA=ya maskini”
Hivyo basi mwana-punda huyu alikuwa amefungwa katika mazingira magumu,kama ilivyo kwa mtu aliyefungwa,

mara nyingi mtu hufungwa katika mazingira magumu,Lakini ipo Neema yake Bwana Mungu siku ya leo,
maana Yeye anasema aliyachukua masikitiko yetu na kwa kupigwa kwake sisi tumepona (1 Petro 2 :24 ).

Yeye Mungu mwenye kuweza kuona mbali kwa habari ya mtu aliyefungwa kama vile amuonavyo mwanapunda,aweza kukuona wewe tokea mbali utoke katika hivyo vifungo.

Kumbe wapo wanapunda waliofungwa hata hivi leo.
Bwana huwafungua waliofungwa na magonjwa kwa sababu ana haja nao.
Bwana huwafungua wote wanaoteswa na mapepo kwa sababu ana haja nao.
Bwana huwafungua wale wote walio na uchumi mbovu kimaisha kwa sababu ana haja nao.N.K

• Kwa ibada ya maombezi au hata kujuliana hali, mawasiliano yangu ni 0655 111149

ITAENDELEA
UBARIKIWE.

Comments