IJUE DHAMBI INAVYO MWINGIA MTU SEHEMU 2

 na MWINJILISTI ISAYA CHIBULILU WA ZANZIBAR


Tunaona Yesu anatufundisha kuwa kilicho nje ya mtu hakiwezi kumtia mtu unajisi bali kimtokacho. Sasa endelea;

Mwanzo 4:3-10 tuangalie mstali wa tano ''''Bali kaini hakumtakabali wala sadaka yake, kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. 6. Bwana akamwambia kaini, kwanini una ghadhabu? na kwanini uso wako ume kunjamana? 7. kama ukitendavyema, hutapata kibali? usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamaniwewe,walakini yapasa uishinde''''' Hapa tumeona baada ya Mungu kuikataa sadaka ya Kaini, Kaini alighadhibika, kwa hiyo hasira ilitoka ndani ya Kaini. Na Mungu akamwambia kuwa kwanini umeghadhibika? [yaani unahasira?] Mungu akamwambia ukiacha kutenda ni vema. kwa hiyo maamuzi yalitoka ndani ya kaini na alipewa onyo kabla ya kutenda. Mstari wa 8. '''''Kaini akamwambia Habili nduguye, (twende uwandani) ikawa walipokuwapo uwandani Kaini akamwinukia Habili nduguye akamuua''' kwa hiyo tumeona hata kabla ya Kaini na Habili hawajaenda uwandani, Kaini ndani ya moyo wake kulikuwa na na roho ya uuaji kwa lugha nyepesi dhambi ilikuwa mlangoni. wakati anatekeleza lile tendo dhambi alikuwa anayo tayari ndani ya moyo wake.

kumbuka katika injili Yesu alisema ukimtizama mwanamke kwa nia ya matamanio tayari umesha zini naye kwa maana maamuzi yanatoka ndani.
Marko 7:20 aksema kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila ufisadi,kijicho, matukani. Hayo yote yaliyo maovu yatoka ndani. Hivi ndivyo dhambi imwingiavyo mtu.

Sehemu ya tatu ya somo letu tutaona Mungu anatuagiza tuishinde dhambi.
KAMA AMBAVYO ALIMWAMBIA KAINI USIPOTENDA NI VYEMA.

MWINJILISTI ISAYA CHIBULILU
                        ZANZIBAR

Comments