![]() |
MWIINJIlISTI ISAYA CHIBULILU ZANZIBAR |
Mwanzo 3:1-13 Nitazungumzia mst 6 mwanamke alipoona ya kua ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
Huyu mwanamke alipo ona wafaa tayari dhambi ilimwingia kwa sababu YESU KRISTO anasema katika Marko 7:15-16 kuwa ''hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu'';
Hawa kilicho mtia unajisi ni kilichotoka ndani ya moyo wake kwakua aliona tunda latamanika, lafaa kwa chakula, ndicho kilicho mtia unajisi, kwa hiyo tunda lilikuwa lipo nje ya Hawa, kwa maelezo ya YESU sio lililo mtia unajisi, bali ni kile kilicho mtoka yaani alipoona lafaa kwa chakula.
Marko 7:18 '' Akawaambia, hivi hata ninyi hamna akili? hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi''
TUNDA lilimwingia Hawa kwa hiyo kilicho mtia unajisi ni kilicho toka ndani ambacho ni kile alicho kiwaza, hivyo basi dhambi inaweza kukupata kwa maamuzi ya ndani ....
ndugu
somo hili litaendelea ...nakalibisha maswali ndani ya somo hili
MWIINJIlISTI ISAYA CHIBULILU
ZANZIBAR
Comments