Isije Ikawa Umembeba Yona!

HadithiyaYona
Kwenye Biblia, katika Kitabu cha Yona, tunapata habari za watumishi wa ile Melikebu aliyopanda Yona, jinsi walivyohangaika baharini, wakatosa mizigo yao wakitafuta ufumbuzi wa namna ya kupita katika ile dhoruba lakini haikusaidia. Walipomtosa Yona Baharini DHORUBA ilitulia, wakafanikiwa kuendelea na safari yao.
Yawezekana unafanya kazi pamoja na mtu, au unashirikiana naye. Lakini mambo yamekuwa hayaendi. Kabla hujawa naye mambo yalikuwa sawa tu, lakini sasa DHORUBA ni kubwa. Unajaribu kuacha baadhi ya mambo/Majukumu ili muweze kujikita katika machache lakini bado haisadii. Kaa chini.
Omba Mungu akufunulie. Wale jamaa wa kwenye melikebu walipiga kura, ikamwangukia Yona. Yawezekana uliye naye hapo AMEKIMBIA KAZI YA MUNGU/WITO ama kwa kujua au kutokujua. Pengine alitakiwa achunge Kanisa au alitakiwa awe mahali fulani akiihubiri Injili. Utashangaa, mkigundua kusudi la Mungu lililo nyuma ya matatizo mnayopitia, amani itapatikana na SHUGHULI yako Itasimama Imara Tena!

Comments