JINSI YA KUUSHINDA ULIMWENGU NA TAMAA ZAKE.

Mwl Nickson Mabena akifundisha neno la MUNGU na hapo ni Mruvango, wilayani Siha mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha.


nmekutana na watu (hasa vijana) wanatamani kuishinda dhambi, kwan wengine wanashindwa kumtumikia Mungu wa mbinguni kwa uhuru... kwan dhambi imetawala maisha yao ya kila siku.

Yafuatayo ni mambo ya msingi ya kumsaidia mtu ili kuushinda ulimwengu;

1. UWE AMEOKOKA.
Kuokoka ni kumkaribisha Yesu Kristo moyoni mwako ili awe Bwana na Mwakozi wa maisha yako.
Yesu ndiye anayeweza kukushindia dhambi, kwani peke yako haiwezekani (YESU NDIYE ATUSHINDIYE).
Rumi 10:9,10. Marko 16:16

"Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami" Ufunuo 3:20

2. UWE UMEJAA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE.
-Roho ndiye hutupa nguvu ya kushinda baada ya kuokoka.

"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu Roho Mtakatifu;" MDO 18a

- Roho ndiye msaidizi wa mwanadam (BILA YEYE HAWEZI)

"Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine,....." Yoh 14:16,26

3. UWE NA NENO LA MUNGU LA KUTOSHA.

"Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa Zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neemaa mioyoni mwenu" Kol 3:16

--Litafakari mchana na usiku (Yosh 1:8)
Yesu alimshida shetani kwa NENO (Luka 4:1-)




4.UWE MWANA MAOMBI.

Luka 18:1, Math 26:36-44
Math 7:7-8.
MUNGU akubariki sana
By Mwl Nickson Mabena

Comments