"JITAHIDI SANA KUMUOMBA MUNGU ILI MANENO YA KINYWA CHAKO YAPATE KIBALI MBELE ZAKE"

Abel Suleiman Shiriwa

Watu wengi sana hutazama dhambi zenye kufahamika ki urahisi na zenye kuonekana kwenye Macho ya watu hupesi, kama vile:-
UZINZI
ULEVI
USENGENYAJI
UWONGO
MATUKANO.

"Wakijua kuwa wakijizuia kwa hayo basi watakuwa wako salama mbele za Mungu"
Lakini kumbe yako mengine ambayo anaweza kuyatamka > kuyafanya, bila kujua kuwa hakupaswa kuyatamka au kuyafanya, na akitegemea kuwa MUNGU hawezi kuyahesabu, lakini sivyo, Msikilize Yesu anavyosema:
Mathayo 12:33-37 ''Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake kuwa mabaya kwa maana kwa matunda yake Mti watambulikana, Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana kwa kinywa cha mtu huyanena yale yaujazayo moyo wake, Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya. Basi, nawaambia, kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa..
"Kwa hivyo Maneno yako lazima uwe makini nayo, unaweza kujikuta siku ya Hukumu unaenda Jahanamu kwa sababu ya maneno yako yasiyo maana ambayo hukujua kuwa hayana maana kwako"
Watu wana masihara mengi, wakijua ni hali ya utani, kama vile kumwita mwenzio:
Fala,
Bwege
Mkuda,
Mbulula
Nk.

Yote hayo yanaandikwa, na siku ya hukumu utakuja kuyatolea hesabu,
Zingatia Maneno ya Yesu, katika aya 37
"Kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa Maneno yako Utahesabiwa hukumu"
'MUNGU AWE PAMOJA NAWE KATIKA HATUA HIYO YA KUYALINDA MANENO YAKO'
"AMENI".

Comments