Kanisa la Kilutheri Marekani lapata Askofu Mkuu mwanamke!!


liz

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Marekani (ECLA) tarehe 14/08/2013 limemchagua Bi. Elizabeth Eaton kushika nafasi ya uaskofu mkuu,  alipata kura 600 dhidi ya anayemaliza muda wake Askofu Mark Hanson, ambaye alipata 287.

Askofu Eaton, ambaye ni Askofu wa ELCA Cleveland, ni mama na mke wa Mchungaji Conrad Selnick. Mtumishi Eaton anaungana na Askofu  Jefferts Schori Katharine, ambaye mwaka 2006 alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuliongoza kanisa la Anglikana duniani.

Eaton ataongoza kanisa kwa miaka sita (6) kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.

“Bwana analitoa Neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa” Zaburi 68:11

Comments