KUMFUNGA SHETANI;

Na Nehemia Msaghaa
Kwa kuwa vita yako ya sala inahitajika haraka sana na shetani ana nguvu sana,tumetakiwa kuvaa silaha zote za MUNGU ambazo anatoa ili tupate ushindi.(Efe 6:13).(Efe 6:19-20)inaongelea vita vyote vya kiroho.Na tukiangalia katika (Efe 6:11) inatuonyesha silaha zote za kuweza kuzipinga hila za shetani.
Kanuni zinazoweza kutumika ili kumfunga shetani ni kama ifuatavyo:


1;  FURAHIA USHINDI WA KRISTO DHIDI YA SHETANI PALE KALVARI NA PEPO WAKE WACHAFU.

Itie nguvu sala yako kwa kusoma maandiko(Lk 10:19),(Yona 12:31-33),Rum 16:20, (1 kor2:6),(Efe 1:21-22),(kol 2:15),(Ebr 2:14),(Yakobo 4:7).Mpe MUNGU sifa kwa ajili ya ushindi mkamilifu wa KRISTO.

2;  FURAHIA KATIKA MAMLAKA NA UWEZO MKUU WA KRISTO-

Mpe MUNGU sifa kwa kuwa YESU ameketi mkono wa ukuu huko juu(EBRANIA 1:3).

3;  OMBA DAMU YA YESU.
Usiweke imani juu yako mwenyewe bali juu ya damu ya YESU (RUM 3:25).


4;  TUMIA JINA LA YESU-Vita vyako vya sala ni kwa ajili ya jina lake.Naye aliahidi,Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu,hilo nitalifanya,Ili BABA atukuzwe ndani ya mwana.(Yn 14:13-14).Lolote mmombalo Baba kwa jina langu awapeni(Yn 15:16).


55;  TUMIA JINA LA YESU UNAPOSALI-Litumie pale unapochukua hatua ya kumsukuma nyuma shetani na pepo wake wachafu.


6;  CHUKUA UPANGA WA ROHO,NENO LA MUNGU-YESU mwenyewe alitumia Neno kumshinda shetani(Mt 4:1-11).Silaha ambayo ROHO MTAKATIFU huitumia kumshinda shetani,Upanga wa Roho ni Biblia(Efe 6:7).


7;  SONGA MBELE HUKU UKIMSIFU MUNGU.
Sifa pia ni silaha yenye nguvu sana ya kiroho.Yehoshafati ndiye mfalme pekee ambaye alishinda vita halisi kwa sifa badala ya silaha(2 nyakati sura ya 20).


8;  TUMIA SIFA KUMSHINDA IBILISI-Sifa huimarisha roho yako mwenyewe ya imani.Maana kusifu kunawaleta malaika wa MUNGU kukusaidia katika matatizo yako.


9;  MWAMURU SHETANI KATIKA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI ALIYE HAI-Mwambie shetani,ulishindwa pale kalvari.Kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO nakuamuru ondoka.Kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETHI ALIYE HAI ninakufunga wewe na kazi zako zote.


MSHUKURU MUNGU KWA KUKUSHINDIA.sema AMINA.

  -Nehemia Msaghaa

Comments