KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU


Bishop YONA   P  SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL

0754049163

(Kiongozi ni wa muhimu sana, Kiongozi lazima ajue njia (Roho anajua Zab: 32: 8a)

 - Mungu anatumia njia mbalimbali kuongoza watu wake
-Jinsi ya kuongozwa na roho.



A.   Watu wengi wanajikuta katika hali ambazo hatujui tufanye nini lakini Mungu anayo majibu kwa ajili yetu.

-Mungu amepanga wale walio katika Yesu waongezwe na Roho wake.

-kama tunataka tuone mafanikio katika maisha yetu, lazima maisha yetu      yaongozwe na Roho na yawezeshwe na Roho.



B.    Mmojawapo ya mambo yenye kuvunja moyo mno hapa duniani ni watu kuwa katika wokovu lakini wasijue jinsi ya kuongozwa na Roho.



Mungu ametupa Roho wake ili atusaidie tufanye maamuzi sahihi.

1.     Tunapokabiliwa na mateso.

2.     Kuudhiwa.

3.     Mashambulizi ya Kiroho

4.     Shinikizo la mawazo.


-Tunapotaka kununua ardhi, kujenga ,kuwasaidia watu, kuhubiri ,kuoa ,kuolewa, kusema, kunyamaza yaongozwe na Roho.

-Tunahitaji msaada wa Roho wa Mungu sana.

- Roho yupo kutusaidia tufanye vizuri (Rum 8:26)

-Roho hukaa kwa mtu mtii na mnyenyekevu (Mat 5:32)

-Tumepewa Roho wake ili tufanye maamuzi yanayofaa.

-Ni vizuri tujifunze jinsi ya kumsikiliza Roho wa Mungu.

-Ili uwe mwana wa Mungu kubali kuongozwa na Roho wake (Rum 8:14)

- Kama huna Roho wewe siyo wa Yesu (Rum 8: 9)

- Maamuzi uliyowahi kuchukuaga uliongozwa na Roho, kazi uliyonayo au uliyowahi kuifanya ukaacha uliongozwa na Roho?

- Maamuzi tunayofanya bila kuongozwa na Roho yatatugharimu sana.

 -Kadri ulimwengu unavyoendelea na mambo yake, sisi tunapaswa tumsikilize Mungu sana.

- Andiko toka:- Torati 4: 5-6 Neno ni hekima hekima zetu na akili zetu.



MUNGU ANATUONGOZA KUPITIA NENO LAKE LILILOANDIKWA:



- Neno la Mungu lililoandikwa ni Hekima ya Mungu (Luka 11: 49)

- Je unahitaji hekima ya Mungu kwa ajili ya maisha yako au nyumba yako, kazi yako, Biblia ndiyo mahali pa kwanza pa kutafuta.



A.   Watu wanapokosa mwelekeo wataupata kwenye neno la Mungu.

Neno la Mungu liliandikwa linatuhakikishia Kufanikiwa katika maisha yetu kile tunachotaka kukifanya (Yosh 1: 7-8)

Mungu alimpatia mwelekezo ili huduma yake iwe na mafanikio.



Mwana alimwambia ulitafakari neno lake usiku na mchana.

Tafuta majibu yote ya maisha yako katika neno la Mungu.

Ayubu alilitunza neno la Mungu kuliko riziki yake (Ayubu 23:12).

Neno linamulika njia yetu (Zab 119: 105 , 128 Mf, Mama Jusi na nyota.

Mungu anatuongoza kwa neno lake.



B.    Ukitaka maisha yako yapendeze na kufanikiwa weak maisha yako juu ya neno (Mawazo, maamuzi, utendaji) Zab 119: 9-10.

Roho awaongoza katika kweli yote ya neno la Mungu (Yoh 16: 13, 17: 17).



C.   Tafuta kwanza neno la Mungu linasemaje kabla yaw ewe kufanya maamuzi.

Mf, Ibrahim na Lutu/ alifanya maamuzi kuondoka na ndugu yake akamwuliza Mungu, Lutu alikuwa shida na watumishi wake katika safari, ugomvi kila siku.



Huyo rafiki uliyenaye ulimpata kwa Mungu, mfanya kazi, mume, mke kwa uongozi wa Mungu.

Wakati tunapoenda kando na neno ndipo tunatumbukia.



MUNGU ANATUONGOZA KWA AMANI YAKE NDANI YETU (KOLOSAI 3: 15)



- Tujifunze kuruhusu amani ya Mungu ikuongoze (acha ijenge ngome ndani yako).

 - Amani iamue na mkate shauri kikamilifu yanayoinuka katika nia ya akili zenu.



 -Unapoanza kuomba kuhusu kufanya jambo, jiulize kama una amani moyoni mwako au unasitasita huna hali ya kutulia.



 -Unataka kufanya biashara, kusomea ujuzi Fulani, unataka kuoa/kuolewa na Fulani n.k.



 -Ukienda katika njia ya hekima kutakupelekea kwenye amani (Mith 3: 13 – 17).



 -Jua majaribu ya Mungu ni amani (Njia zote Mungu aweza kupitisha matumaini hata kama zina mateso).



 -Maamuzi mengi makubwa yanaweza kufanywa kwa misingi ya Amani.



  -Roho wa Mungu aweza kukataza au kukuzulia jambo Fulani uwe makini mf, (Mat 16: 6).
ITAENDELEA...


MUNGU akubariki sana
 by Bishop YONA   P  SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
karibu kwa maombezi na ushauri wa kibiblia

Comments