KWA NINI TUWAAMBIE WATU HABARI ZA WOKOVU!?

Mwl Nickson Mabena

1.Tumeagizwa na Yesu (anayeokoa) tufanye hivyo.
(Marko 16:15,16, Mdo 1:8)

"Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa." Marko 16:15-16


2.Kwa sababu ya upendo aliotuonyesha Mungu.
(2Kor 5:14, 1Yoh 4:19; Rumi 5:5)

"na tumaini halitahayarishi; Kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi" Rumi 5:5
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" Yoh 3:16



3.Kwa kuwa mwisho wa wasioamini ni moto wa milele.
(Rumi 6:23; 1Yoh 5:12; Ufunuo 20:15)

"Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" Rumi 6:23
"Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto" Ufunuo 20:15



4.Wewe (Uliyeokoka) ni shahidi jinsi Mungu alivyobadilisha maisha yako. (Kkwa upande wangu, mimi ni shahidi)
"Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu." 1Petro 3:15

MUNGU awabariki sana .
Mwl Nickson Mabena

Comments