MAFURIKO YA WATU, ZOEZI LA KUAGA LASITISHWA KWA MUDA

Jeneza lililohifadhi mwili wa marehemu, Askofu Mkuu, Moses Kulola. ©Philemon Rupia/WAPO Media
Kutokana na maelfu ya watu kujitokeza kwa wingi kumuaga Askofu wa Maaskofu, Baba/Babu wa kiroho kwa wengi nchini, zoezi la kuaga mwili wake limesitishwa kwa muda kutokana na idadi ya watu kuelemea eneo la tukio, kwenye kanisa la EAGT Temeke.

Gospel Kitaa imeshuhudia kila mtu akijitahidi kw akadri ya uwezo wake kufika eneo ambalo jeneza lipo ili apate kutoa heshima zake za mwisho, lakini umati wa watu kufanyika kizuizi, ambapo pia hitilafu ya mitambo iliyopelekea vipaza sauti kuzimika, imechangia kupungua kwa ufanisi wa mawasiliano eneo hilo.

Huenda zoezi likasitishwa kabisa iwapo mambo hayatokaa sawa, ila kwa kadri waratibu wanavyoweka mambo sawasawa, nafasi ya kuendelea kuaga inatumainiwa zaidi na kila aliyeacha
shughuli zake kutokana na umuhimu wa hayati kwenye maisha yao.

                CHANZO NI GOSPEL KITAA

Comments