MAISHA YA WOKOVU YAKOJE?


PETER MICHAEL MABULA



-Wokovu ni maisha ya ushindi dhidi ya dhambi
-Maisha ya wokovu ni maisha anayoishi  mtu aliyezaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
-Wokovu ni kuishi maisha ya kitakatifu.
Yohana 3:1-7’’………..mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuingia ufalme wa MUNGU……’’

-TUNAZALIWAJE MARA YA PILI?

tunazaliwa kwa neno la MUNGU lenye uzima lidumulo hata milele. 1 Petro 1:23-25''

Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la MUNGU lenye uzima, lidumulo hata milele. Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka; Bali Neno la BWANA hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu. -Baada ya kuokoka tunatakiwa tuukulie WOKOVU.1 Petro 2:2''
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; '' na tunatakiwa pia tuishi maisha ya wokovu maana tutapataje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii yaani tunaokolewa bure kabisa kupitia YESU KRISTO .Waebrania 2:3.''
sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na BWANA, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;  
- Ndugu Wokovu(kuokoka) ni muhimu sana na bila wokovu kuna adhabu Waebrania 10:27-29.'' bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. .....  Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa MUNGU, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema? ''
-Ndugu wokovu umeletwa na BWANAYESU na yeye mwenyewe amesema tukimkataa yeye tumekataa uzima wa milele .Yohana 12:48-50.''
Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo. ''
-Ndugu ukiamua kuokoka okoka kwelikweli na mwangalie mwenye kuanzisha na kuitimiza imani yako (Waebrania 12:2)-
tukimtazama YESU, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha MUNGU.   maana wapo pia  wanaoigiza kuokoka na pia wapo pia ambao wanakataa kuokoka duniani kana kwamba wakifa kuna tukio watalifanya wakiwa marehemu ambalo litawaponya. Watu hao jiepushe nao.Tito 1:16 '' Wanakiri ya kwamba wanamjua MUNGU, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai. '' na pia katika Ezekiel 33:31''  Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao. '' Biblia inasema.
-Ndugu MUNGU anawajua walio wake na wewe ukimpa YESU KRISTO maisha yako na kuishi katika utakatifu au kuishi katika maisha ya wokovu hakika utakua katika kundi hili la wateule waliosafishwa kwa damu ya YESU tena wamezaliwa kwa neno la MUNGU .Hivyo ni wajibu wako na wangu kutimiza wokovu wetu.Wafilipi 2:12 '' 
Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. ''.
-Ili uishi maisha ya wokovu ni lazima kwanza umpe YESU maisha yako yaani uokoke.
-Kuokoka ni kufanyika mtoto wa MUNGU. Ili uokoke ni
(A)Lazima umkiri YESU KRISTO kuwa mwokozi wako (Warumi 10:9-10) Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

  (B)Ujue kuwa YESU alikufa kwa ajili yako ili usamehewe bure kupitia yeye.(Wagalatia 2:20)
Nimesulibiwa pamoja na KRISTO; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali KRISTO yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa MUNGU, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

  (C)Lazima kutubu dhambi zako zote(Marko1:15) Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. .
MUNGU awabariki sana na hakikisha unaishi maisha ya wokovu maana YESU KRISTO alikuja ili wewe na mimi tuwe na uzima kisha uzima wa milele.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.

Maisha ya ushindi Ministry.
0714252292

Comments