MAJARIBU NA AINA ZAKE


       
-Majaribu ni kushawishi  kutenda  kinyume na  mapenzi  ya MUNGU
-Ni  kipimo  kwa  mtu  yaani  yuko  imara na anafaa? 
‘’Heri  mtu  anastahimilie  majaribu  kwa  sababu  akiisha  kukubariwa  ataipokea taji  ya uzima  BWANA aliowaahidi  wampenda{1 petro 6;7}
‘’Mnafurahi  sana  wakati  huo  ijapokuwa  kwa  kitambo  kidogo  ikiwa  ni  laazima  mmehuzunishwa  kwa  majaribu  ya  namna  mbalimbali 
 
- KINACHO JARIBIWA  NI NINI?
 - Ni imani  ya mtu  

-ANAYESABABISHA JARIBU.
1-Mtu kujua  au kusababisha  mwenyewe 
2-Watu  wengine  kusababisha  jaribu  hilo

AINA ZA MAJARIBU

1-MUNGU  mwenyewe {zaburi 11:5} 
‘’BWANA  humjaribu  mweyehaki  Bali nafsi  yake  humchukia  asiye  haki   na  mwenye udhalimu’’ {mwazo 22:1-2-Ikawa baada ya mambo hayo MUNGU alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.  Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia. }    {mithali 17:3} 
{…….bali  BWANA humjaribu  mioyo } na {waebrania 10:32-33 Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu; pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na dhiki, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo.


2-  Mtu  mwenyewe  binafsi  {wagaratia 5:16} 
‘’Basi  nasema  enendeni  kwa  roho  wala hamtazitimiza  kamwe  taama  za  mwili ‘’
-Tamaa  ya mtu  inaweza  kuwa  jaribu
-Kuwepo  mahali  kwa  wakati usio  sahihi inaweza kuwa jaribu kwako  {2samweli 11:1-12} {waefeso  5:15-16 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. }
-Tabia  ya  mtu  mwenyewe  {mithali 6:25-26-Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani } Pia {mithali 15: 1-2}‘’Basi  umetengwa  kwa  maneno  ya  kinywa  chako  umekamatwa  kwa  maneno  ya kinywa  chako 
Maana  kwa  Malaya  mtu hutiwa  katika  hali  ya  kuhitaji  kipande  cha   mkate na  kahaba  humwinda  mtu  anasema  nafsi  yake  iliyo  ya  thamani.
Jawabu  la  upole  hugeuza  hasira  Bali  neno liumizalo  huchochea  ghadhabu,ulimi  wa mwenye hekima  hutamka  maarifa  vizuri  Bali  vinywa  vya  wapumbavu  humwaga  upumbavu 


3- Jaribu  la  shetani  {massa}  {1wathesalonike 3:5}
‘’Kwa  hiyo  mimi  nami  nilipo  siwezi kuvumilia   tena  nalituma  ili  niijue  imani  yenu  asije  Yule  mjaribu  akawajaribu  na  tabu  yenu  ikawa haina  faida      
  {mathayo 4:3 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. } ,{1kor 10 :13Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. } {yohana 16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. }


KWANINI TUJARIBIWE?

a.  tunajaribiwa ili  kuangalia uimara wa imani yetu. 
  
 b.  kutaka kutunyenyekesha 

c.  ili  kumtambua  MUNGU {danieli 3:28-29} {1perto 1:12}  {luka 23: 47-48} 

TUFANYE NINI WAKATI WA JARIBU

1: Inatupasa  kufurahi   {nehemia 8:10} 

2: Maombi  {mathayo 26:4 }  
‘’kesheni  mwombe msije mkaingia majaribuni roho radhi lakini mwili ni dhaifu

3: usiwe  mtu  mwenye lawama{2 timotheo 4:16-17 Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini BWANA alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. }.
Hitimisho langu ni hili {Yakobo 1:13-15-Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na MUNGU; maana MUNGU hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. }.
 ndugu zangu wapendwa watu wengi sana wamekuwa kwenye majaribu na kudhani kuwa wanajaribiwa na MUNGU kumbe ni tamaa zao wenyewe maana MUNGU hawezi kumjaribu mtu kwa uovu na pia  na MUNGU anapomjaribu mtumishi wake kwanza huyo mtumishi anakuwa katika hali nzuri kiroho yaani amejaa Roho wa MUNGU sio wale ambao kwa tamaa zao wenyewe wanadhani wanajaribiwa na MUNGU pia wengine kwa sababu ya kupungukiwa na maombi wanajikuta wanajaribiwa huku wao wakidhani wanajaribiwa na MUNGU kumbe walilala tu usingizi wa kiroho ndio maana wako katika majaribu hayo.
MUNGU akubariki sana ndugu na pia kama hujaokoka nakushauri leo chukua hatua za kumpa BWANA YESU maisha yako ili ufanyike mtoto wa MUNGU na uwe mbali na kuonewa na shetani na mawakala wake majini, wachawi na kila aina ya kazi za shetani.
YESU KRISTO BAWANA wa utukufu anakupenda sana
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
                    maisha ya ushindi

Comments