![]() |
LILY PETER NA MWANAYE TROY |
BWANA
asifiwe mtumishi! usiku nimeshuhudia kitu kwa macho yangu sikuwa katika
ndoto,ilikua usiku wa saa tisa na dk 35 mtoto alikua ameamka analialia
nikawa nambembeleza lakini hanyamazi cha ajabu kuna mtu alitokea kitandani
ghafla akamgusa mtoto baada ya kumgusa, mtoto akaanza kupaa huku
amesimama na kitandani kikabaki kivuli,nilijaribu kuongea
nilishindwa,nikawa namwita mume wangu sauti haitoki,nikitaka kutaja jina
la YESU nashindwa,nikaamua kusali kimoyomoyo nikaona mikono ya mtu
mwingine sikujua ni nani ila alikua anamsaidia mtoto asipae! naamini
alikuwa malaika wa BWANA alikuja kumzuia asipae baada ya mimi kusali,pia
naamin hawakumchukua kwasababu MUNGU alionyesha muujiza wake.
By Lily Peter
By Lily Peter
Kutoka maisha ya ushindi.
MUNGU
akubariki sana na vikwazo vya shetani vipo lakini MUNGU wetu ni mshindi
tu siku zote ninachokuomba endelea na maombi na pia watu hao wana
mpango mbaya na mtoto wako ila MUNGU yuko upande wako kukutetea maana
umemtegemea yeye hata hivyo ukiweza nenda kanisani kwa maombezi zaidi au
hata ukiweza unaweza kuja kanisani kwetu hata leo mchana tukakuombea na
MUNGU wa miujiza akatenda muujiza wake na pia hata sisi kuja huko ili
kukuombea inawezekana sana. MUNGU akubariki pia ushuhuda wako huu naomba
kama ukiniruhusu niuweke kwenye blog na page yetu ili wengi zaidi
wajifunze kumtegemea MUNGU kama ulivyofanya wewe na MUNGU akamtuma
malaika wake ili kukuokoka wewe na mtoto wako lakini haya ni mpaka wewe
mwenyewe uruhusu. ubarikiwe sana
Kutoka kwa Lily Peter
Amina mchungaji,hakika Mungu ni mwema! Unaweza kuuweka hakuna tatizo
Kutoka maisha ya ushindi.
amen ndugu yangu japokua mimi sio mchungaji ila ni muumini tu. Hata hivyo MUNGU akubariki sana na kila kusudi la shetani dhidi yako na mtoto wako halitafanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Nakufunika kwa damu ya YESU KRISTO na pia nakuomba kumbuka tu kuokoka ni jambo muhimu sana hivyo unaweza kutafuta kanisa huko huko uliko ambalo ni kanisa la kiroho na ukiwaeleza watakusaidia. pia kama ukipenda naweza kuwaambia wadada kama wewe watatu wakaja wakaomba pamoja na wewe huko kwako. MUNGU akubariki sana na aendelee kukutetea siku zote na Troy akue katika KRISTO amkimbpendeza MUNGU na wanadamu. AMEN
![]() |
TROY NA MAMA YAKE |
Comments