MTUMISHI WA MUNGU ANATAKIWA AWE NA SIFA HIZI


Mungu anatutaka tunapomtumikia tuwe na sifa za kuwa watumishi wake ili jina lake lisije likatukanwa.

1. Kuongozwa na Yesu Kristo


1Korinto 2:2 Maana nalilazimu nisijue neno lolote kwenu ila Yesu Krito, naye amesulibiwa.


2Korintho 4:5-6 Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo aliye sura yake Mungu. Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu yakuwa ni Bwana; na sisi wenyewe tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.


2. Kuongozwa na neno la Mungu


2Timotheo 3: 15-17 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Krito Yesu. Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.


Ebrania 4:12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


3. Kujazwa na nguvu ya Roho mtakatifu


Matendo 1:8 Nanyi mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.


2Korinto 3:5-6 Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lolote lwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua bali roho huuisha.


4. Kuwa na sifa njema


1Thesalonike 1:5b-6 kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa sifa zetu kwenu, kwa ajili yenu. Nanyi mkawa wafuasi wetu na Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.


5. Mwenye kuongozwa na upendo


1 Thesalonike 2:8 Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili tu,bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.


1Korinto 13:1-3 Nijaposema kwa ligha za wanadamu na malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha masikini, tena nikijitoa mwiliw angu niungue moto, kama sina upendo hainifaidii kitu.


6. Moyo wa Utumishi


2Korinto 4:5 Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.


1Korintho 4:1-2 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.


7. Aliyejaa maombi


Wafilipi 4;6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.


8. Imani thabiti


Luka 1:45 Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.


Ebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa dhawabu wale wamfuatao.


9. Furaha ya kweli


Zaburi 100:2 Mtumikieni BWANA kwa furaha, njooni mbele zake kwa kuimba;
MUNGU akubariki
by
Conrad Conwell

Comments