MUNGU ANATUONGOZA KUPITIA USHAURI WA WENGINE (Mith 20: 18, 24:6).




Mungu ametupa mwili wa Kristo ili kutusaidia.

A.   Hakuna mwanaume  au mwanamke aliye kisiwa, yaani asiwe na mahusiano na wengine (Huwezi kujitosheleza mwenyewe unahitaji mwingine akushauri) Zab 32: 80 nitakushauri.
B.    Wewe peke yako ndiye utakaye wajibika kwa Mungu kwa maamuzi yako.

 - Katika maamuzi yako mabaya yasiyohitaji ushauri au kukataa ushauri utaumia.
 -  Mf, Samsoni alishauriwa lakini alikataa mashauri (Waamuzi 14: 1-3).
 -  Watu wengine wanaweza kutusaidia kuona mambo kwa namna mpya kabisa kuliko tunavyoona au kusikia hasa wakati wa msongo wa mambo mengi.

 -  Tilia maanani unapoambiwa jambo ambalo hujawai kuwaza katika hilo jambo.

Vijana wengi hawaongozwi na Roho – ndiyo maana ndoa nyingi zinaishia pa baya.
 -  Ndiyo maana mmoja anapoingia kwenye ndoa alikuwa na safari ya kwenda mbinguni inageuzwa anaanza kwenda jehanamu, (Ugomvi usioisha).
 -  Washauri wanasaidia mtu kuchunguza nia na makusudi yake na ili azingatie muda unaofaa.
Uwe makini sana kupokea ushauri kutoka kwa wengine, (Mf, Musa na Mkwewe).
 -  Ni lazima tuwe wazi kwa wale wanaotupenda , (Mith 18:1) tusijitenge na wengine, tusishindane na kila ushauri.
 -  Ukiwa umeshauriwa vizuri kubali na kama ulishakusudia jambo kubali kweli sahihi.
  - Yale maamuzi tunayofanya yawaadhiri wengine zingatia:-
a.      Angalia neno la Mungu.
b.     Ukamilifu katika amani ya Mungu  ndani yetu.
c.     Ushauri wa wengine.

MUNGU awabariki sana
 by Bishop YONA   P  SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
karibu kwa maombezi na ushauri wa kibiblia

Comments