MUNGU KATUPONYA NA HATARI!

na Mtumishi wa MUNGU Pastor Peter Mitimingi.



Ni saa Tisa usiku sasa hapa Chicago
Nikiwa nimelala ghafla nikasikia alam ya hatari ikilia hotel nzima nikakurupuka nikavaa kidogo nikadhani kuna kitu kime leta shoti labda chooni kwangu. Kwenda chooni hakukuwa na tatizo ila kelele za alam ya hatari zikawa zinaendelea nikaamua kupiga simu receiption simu ikawa haiendi nikaamua kupia simu ya dharura pia sikufanikiwa. Nikaamua kuchungulia kwenye tundu la mlango nikaona baadhi ya watu wanapita pita kwa haraka nikaogopa kufungua mlango kwa hofu ya majambazi labda. Nikabaki ndani ya chumba changu kwa dakika 15 nikiwa naomba na nisijue nini tatizo. Baada ya dk 15 nikaamua kufungua pazia nichungulie kwa nje! WOW! hapo ndipo nilipigwa na mshangao na kuchanganyikiwa. Niliona watu wamejaa nje chini magari ya polisi, fire na kila aina ya askari wa uokoaji wakiwa wamejaa kuja kunusulu na tatizo kutaharuki kumbe watu wote walisha kimbia nje kusalimisha maisha yao mimi peke yangu ndio nilikuwa nimebaki kwenye chumba peke yangu. Nilitoka mbio zisizo za kawaida kutelemka ngazi kutoka ghorofa ya 3 mpaka chini nilitumia sekunde kadhaa nilipepea kama kipepeo wala sikujiona tena kama mzito kufika nje watu wakawa wanashukuru kuniona maana hawakujua wangeniitaje nitoka askari wa ufundi na uokoaje wakiwa wamevalia vifaa maalum vya uokoaji waliingia hotelini na kufanikiwa kudhibiti ile sshort na tatizo kabla halijasambaa baada ya muda hali ikawa shwari ndio tumeruhusiwa tena kurudi vyumbani mwetu. Nilishangaa wengine walitoka nje na vinguo vya ajabu ajabu kweli kwenye kuokoa uhai hujali tena umevaa nini au watu watakuonaje. NAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUPONYA WOTE HAKUNA ALIYE DHURIKA WALA CHOCHOTE. Asante kwa maombi yenu sasa ni saa 10 alfajiri narudo kumalizia usingizi wangu baada ya maombi

Comments