''Mwanadamu ana sehemu TATU ambazo ni ROHO, NAFSI na MWILI, hizi zinachangia katika TABIA YA MOYO wake.

Na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

A: ROHO ambayo inahusisha mambo ya MUNGU.
Ni ile sehemu ya mtu yenye UFAHAMU wa MUNGU, ambayo hufanywa HAI na Hutiwa Nguvu na ROHO WA MUNGU wakati wa WOKOVU. Kabla ya mtu Kuokoka, sehemu hii, haifanyi kazi kwa utimilifu kabisa kwa sababu ya dhambi. Dhambi huifanya kuondolewa Nguvu ya KUTENDA kazi sawa sawa, kwa AMANI na ROHO YA MUNGU. Lakini kupitia UBATIZWA wa ROHO MTAKATIFU, mwanadamu Hupokea NGUVU YA KIROHO, inayomwezesha KUISHI maisha ya KRISTO.

ROHO inahusika na:-
i) Maombi na Ibada na MUNGU,
ii) Ushirika na MUNGU,
iii) Mapokezi ya karama za Roho,
iv) Vita vya kiroho,
v) Kuunda Mawazo na Ndoto,
vi) Dhamira, Kupambanua,
vii) Udadisi, Kuuliza,
viii) Ufahamu, Kutafsiri,
ix) Shuhuda kwa Wanadamu

B: NAFSI inahusika na mambo ya mtu.
Ni ile sehemu ambayo ina ufahamu wa MTU MWENYEWE au kiini cha UBINAFSI wa Mtu. Kazi yake ni:-
i) Kufikiri – Kutafakari, kuona
ii) Hisia – Kujisikia kuwa na tamaa na Upendo
iii) Utashi – Nia, Kuamua

C: MWILI unahusika na mambo ya Ulimwengu.
Ni ile sehemu ya mwanadamu ambayo inafahamu na kukubaliana na ULIMWENGU WA NJE. Inafanya yafuatayo:-
i) Utambuzi wa Ulimwengu, - yaani ile hali ya mwili kupokea habari kutoka Ulimwenguni kwa njia ya Ufahamu.
ii) Urejeshi – yaani ile hali ya Mwitikio wa kutenda kutokana na kutendewa kitu, kupitia utaratibu wa Maneno na Matendo.
iii) Udhihirisho – yaani ile hali ya Mwili ya kutoa habari za Ulimwengu kwa Mawazo, Kujisikia na Maamuzi ya Nafsi.''

Comments