MWONEKANO WA VIJANA MBELE ZA WAZAZI KWA SASA NDIYO SURA YAO YA BAADAYE.

Na Bishop YONA   P  SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.



(Luka 2: 52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu. )
Yesu anaonyesha mwonekano).

(Zab 11:3Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?)

 -Jinsi kijana wa kiume anavyoishi na Mama yake ndivyo atakavyoishi na mkewe.

   -Jinsi Binti anavyoishi na Baba yake ndivyo atakavyoishi na mume wake.


 -Ni mambo machache tu yatakayobadilika au kuongezeka au kupungua.


- Vijana wetu wana nafasi nzuri ya kujitengenezea tabia za kuwasaidia mbeleni wakati wakiwa na wazazi wao au walezi wao.


-  Msingi mzuri unaweza kujenga tu pale ukiwa na wazazi wako (Tabia hujengwa).


- Kijana wa kiume kumjali Mama yake/kumpenda (Mith 4:1-3-Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio mpate kujua ufahamu. Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu.  Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu) kumtia moyo /kumnunulia kitenge / kuwa karibu.


- Binti kumjali Baba yake / kushauriana naye mambo baadhi/kumweshimu.


-  Familia nyingi ambazo zina matatizo mengi pamoja na shambulio la shetani, lakini inategemea kijana wa kiume au wa kike anavyokuwa anaishi na wazazi wake.


- Bwana akiamka asubuhi hajui kumsalimia Baba yake kumpokea.

-  Kijana wa Kiume hajui kumsalimia Mama yake humdharau, hana upendo wowote kwa Mama yake.


- Swala la unyenyekevu linaanzia kwa wazazi pamoja na utii.

-  Kama una tabia umezificha wakati wa uchumba zitajitokeza wakati umeshaolewa au kuolewa.

-  Kama unazo tabia hukuzifanya kwa wazazi wako ambazo zilistahili uwape zitakutesa sana katuka ndoa yako, apandacho mtu ndicho atavuna (Gal 6: 7 Msidanganyike, MUNGU hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. )


-Kama utaolewa au kuolewa jitahidi kuishi vizuri na wazazi wako, jifunze kunyenyekea, kutii, kuwapa pole, asante, nisamehe haya ndiyo maisha ya kila siku.


- Kuwaletea wazazi wako zawadi hata kama ni pipi, tunda nk kwa tabia hapa mnaijenga itakusaidia.
MUNGU awabariki sana by Bishop YONA   P  SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
karibu kwa maombezi na ushauri wa kibiblia

Comments