"NAMBA TATU (3) KIBIBLIA INA MAANA GANI?"

ABEL SULEIMAN SHIRIWA

Kibiblia Namba 3 inamaana zifuatazo:-

(A) NAMBA YA MUUNGANO.

Isaya 6:3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi, dunia yote imejaa Utukufu wake.
Hapa Isaya ametupa habari ya Mtakatifu, iliyorudiwa mara tatu, ikimaanisha Muungano wa Utatu Mtakatifu,
Baba >Mtakatifu
Mwana > Mtakatifu
Roho Mtakatifu.


1 Yohana 5:8-9-Kwa maana wako watatu washuhudiano [Mbinguni, Baba, Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.Kisha wako watatu washuhudiao duniani] Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari Moja...

(B) NAMBA YA USHIRIKIANO

Mathayo 28:19 Basi, Enendeni, mkawafanye Mataifa yote kuwa wanafunzi, Mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

(C) NAMBA YA UKAMILIFU.

Luka 13:32-Akawaambia, Nendeni, mkamwambie Yule Mbweha, leo na kesho natoa pepo na kuponya, na siku ya tatu nakamilika.
Hivyo tatu ilitumikia katika kufufuka kwa Yesu.
Mathayo 12:40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na Usiku katika moyo wa Nchi.
Luka 24:6-7-Hayupo hapa amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa kule Galilaya,akisema, imempasa Mwana wa Adamu kutiwa Mikononi mwa wenye dhambi, na kusulubiwa, na kufufuka siku ya tatu.
Tatu "ILITUMIKA KWA YONA KUKAA KATIKA TUMBO LA SAMAKI.
Yona 1:17 BWANA akaweka tayari Samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye akawa ndani ya tumbo la Samaki yule muda wa siku tatu.
Sauli (Paulo) alifunguliwa na kuona tena baada ya siku tatu.
Matendo 9:8-9
Sauli akainuka katika nchi macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; Wakamshika mkono wakamleta Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali wala hanywi.

Yesu katika muda alioishi Duniani kwa Jinsi ya Mwili, aliitumia Namba Tatu kwa kuwafufua Watu watatu.

(a) Mtoto wa Mwanamke Mjane. (Luka 7:12-17)
(b) Alimfufua binti wa Yayiro.

(Luka 8:41-42)

(C) Alimfufua Lazaro. (Yohana 11:38-44)

HIYO NDIYO NAMBA TATU KIBIBLIA
MUNGU akubariki sana
By ABEL SULEIMAN SHIRIWA

Comments