NGUVU YA MUNGU ITENDAYO KAZI.

Mwl. Sospeter Simon S. Ndabagoye.
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

Kwanza kabisa, tukiri kuwa kuna nguvu ya Mungu ifanyayo kazi; nguvu hiyo ndiyo ilifanya vitu vyote tangu uumbaji wa dunia na viumbe vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana. (Kutoka 20:11),(Mwanzo 1:1-).Hili linatudhihirishia kuwa Mungu alikuwepo tangu mwanzo, na nguvu yake ilitumika katika uumbaji wa dunia na vitu vyote. (Yohana 1:1-4)
Swali la kujiuliza ni je nguvu hiyo kwasasa iko wapi?
Hakika, nguvu hiyo mpaka sasa inaendelea kufanya kazi katika ulimwengu wa roho kupitia watakatifu wake yaani wale waliompokea kufanyika kuitwa wana wake (Yohana 1:12)
Ifahamike kuwa, Mungu alipomuumba mwanadamu, alimuwekea nguvu hii ndani yake kama ushindi na ulinzi ndani yake. Nguvu hii, aliiweka maalumu ili itumike ili kuushinda ulimwengu na majaribu yake! Mungu alifanya hivyo, kama kumtawaza mwanadamu juu ya miliki zote za dunia, na kumpa mamlaka kamili juu ya vitu vyote vilivyo juu ya uso wa dunia (full mandate). Hii ijulikane wazi kuwa Mungu alimuumba mwanadamu nguvu ya Kimungu ndani yake. Hii ni kwasababu, ameumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. (MWANZO 1:27&28) “Mungu akaumba mtu kwa mfanowake, kwa mfano wake, akamuumba mwaume na mwanamke akamuumba. Mungu akwabarikia....akawambia, zaeeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitisha, mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Hii ina maana kwamba, Mwanadamu anlimbwa kwa upendeleo mkubwa, kama mrithi na mwangalizi wa vitu vilivyoumbwa na Mungu.
Baada ya Utangulizi hio, naomba ujue kuwa Mungu hutumia nguvu hiyo hiyo kufanya kazi hata maishani mwako mpaka sasa.
(EFESO 3:20) “basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuwazayo, kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu”
Hii ina maana gani? Maana yake ni kuwa, kuna nguvu au uwezo ambao tayari upo ndani yetu, tena unafanya kazi’Haleluya! Naomba unielewe vizuri, hii inamaana kwamba, Mungu hutumia nguvu iliyoko ndani ya mwanadamu tayari, ili ifanye kazi. Yaani, Mungu hutumia uwezo uliopo tayari ndani ya mtu, ili kuweza kufanya mambo aombayo na hata zaidi ya yale aombayo au awazayo. Ina maana kuwa, unapoomba, Mungu huangalia nguvu iliyondani yako, na hapo ndipo huweza kujibu yale uombayo, uwazayo na hata zaidi yake. Ifahamike kuwa, Mungu hutenda kazi, kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yako! Yaani, kipimo cha Mungu kujibu maombi yako, ni kadri ya kipimo cha nguvu itendayo kazi ndani yako...hii inamaana kuwa, kumbe kuna nguvu inaweza kuwa ndani yako, lakini haifanyi kazi. Pengine niseme kuwa hii ni hasara kwa Mungu, kwa kuwa amewaka nguvu ndani yako ambayo hifanyii kazi yoyote. Hapa Paulo anatujulisha kuwa, Mungu hujibu maombi yetu, kwa kiwango kile tulichoruhusu kifanye kazi ndani yetu. Hii inamaana kuwa, majibu ya Mungu kwetu, hutegemea nguvu iliyoko tayari kufanya kazi ndani yetu. Kwa hiyo, kama unanguvu labda 20, ila inayofanya kazi ni 3, basi Mungu hutumia hiyo 3, huku salio lako ambalo ni 17, likiwa ni hasara kwa Mungu. Ebu chukua mfano muda wa maongezi kwenye simu, unaweza ukawa na salio kubwa, lakini lenye faida kwako ni lile tu, utakalo tumia kwaajili ya mawasiliano. Kadharika nguvu hii ya Mungu ndani yetu, yenye faida, ni ile tu, itendayo kazi ndani yetu. Mfano mwingine ni umeme, kama nyumba yako ina umeme volt kadhaa, wakati matumizi yako ni volt ya chini, basi kumbe, kuna umeme ambao unasukumwa ndani ya nyumba yako ambao hauna faida yoyote, kwa kuwa huutumii. Izingatiwe kuwa, Mungu anatamani, utumia nguvu yote, ili akuongezee nguvu nyingine zaidi. Ebu angalia kwamfano ule ule wa umeme, kama wewe ukifungiwa umeme wa matumizi ya ndani tu, halafu ukahitaji kiwanda, ni dhahiri umeme huo hautakutosha, itakubidi uongeze nguvu zaidi ili kuendeshea mitambo! Hili ndilo ambalo kila mtu, anapaswa kulitamani, ili Mungu amuongezee nguvu zaidi ya kuishinda dhambi. Hata Yesu mwenyewe, kuna kipindi alihitaji kuongezewa nguvu, tunayaona haya katika Luka 22:43 ambapo malaika kutoka mbinguni, walikuja kumtia nguvu, na hapa akazidi kuomba mpaka akawa anaoa nguvu kali sana ambayo ilipelekea ukombozi wa ulimwengu.Luka 22:44, ...hali yake ikawa kama matone ya damu, yakidondoka chini. Hata wewe leo, ukiomba, Mungu anaweza kuiruhusu nguvu zaidi juu yako ili uitende kazi yake, Mungu anawatafuta walioko tayari kuifanya kazi yake, tena kwa uchungu. Kumbuka, Eliya, alijibiwa maombi yake kutokana na nguvu iliyokuwa ikitenda kazi ndani yake, Daniel pia alijibiwa maombi kutokana na nguvu iliyokuwa ikitenda kazi ndani yake!Hata Yesu, aliukomboa ulimwengu kutokana na nguvu iliyokuwa ikitenda kazi ndani yake...waote hawa, walikuwa watu wanaomcha Mungu, wanaomba kwa bidii tena kwa mzigo mzito bila kukoma. Natamani hata wewe leo, uwe na mzigo huo kwaajili ya watu waliopotea, kwaajili ya wanaoteswa na magonjwa, kwaajili ya waliojeruhiwa mioyo yao, kwaajili ya wanaotaka kumwona Yesu katika maisha yao.
Mungu azidi kuwabariki na kuwainua, huku akiwapa roho ya maombi na kujifunza neno lake. AMEN

 Mwl. Sospeter Simon S. Ndabagoye.
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

Comments