NINAYO NDOTO AMBAYO BADO HAIJATIMIA!!!



Muda wangu wa kufa bado kabisa!!
Ninayo ndoto ambayo bado haijatimia, nilishaiona Tanzania imegeuka na kuwa ufalme wa mwanakondoo.
Ninayo ndoto ambayo haijatimia, nilishaiona Tanzania imefunikwa na utukufu wa Bwana kwa namna isiyokua ya kawaida.
Ninayo ndoto ambayo haijatimia, nilishaiona misikiti ya Tanzania imegeuka na kuwa madarasa ya sunday-school za watoto.
Ninayo ndoto ambayo haijatimia nilishawaona mashehe na maimamu wakikimbia mbele ya msalaba wa Yessu kristo.
Siwezi kufa.
Ninayo ndoto ambayo haijatimia niliyaona makaburi yanafunguka kwa uweza wa nguvu za Bwana.
Ninayo ndoto ambayo haijatimia nilishayaona majeneza yamebebwa kutoka nje ya nchi kuletwa huku, kuja kufufuliwa.
Ninayo ndoto ambayo haijatimia.
Nilishaona wahubiri wanainuka Tanzania na kuichoma dunia kwa moto wa Mungu.
Siwezi kufa maana mwota ndoto hawezi kufa mpaka ndoto yake imetimia.
Yusufu hakufa mpaka ndoto yake ilipotimia.
Farao hakufa mpaka ndoto yake ilipotimia.
Mwota ndoto hafi kabla ya ndoto yake haijatimia,
Unaweza kuniwekea sumu kama unavyoweza, unaweza kuleta majambazi kama unavyoweza, lakini mwota ndoto hafi, chombo cha Mungu hakiwezi kurudi mbinguni kabla hakijamaliza kazi yake.

Lazima nimalize kazi niliyotumwa na Baba, na nimepewa uwezo wa kuanza na uwezo wa kumaliza. Na nitaimaliza!!!

Yanipasa kuifanya kazi ya Baba kungali bado asubuhi maana saa inakuja ambayo siwezi kufanya kazi Siwezi kufanya kazi!!

I have a Dream!!!

~Pastor Josephat Gwajima

Comments