Reinhard Bonnke kuanza kuhubiri leo uwanja wa taifa

Shalomu mpendwa,
MUNGU aliyekulinda usiku akulinde pia kuanzia asubuhi mpaka jioni, akupe nguvu tele na afya tele pia kumbuka leo ni siku nzuri sana katika maisha yako endapo utafika katika MKUTANO MKUBWA WA INJILI utakaofanyika UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM kuanzia leo tarehe 21 hadi 25 August 2013 Ambapo Mhubiri wa kimataifa Reinhard Bonnke atahubiri pia kumbuka kwamba mhubiri huyu ndiye anayeongoza duniani kwa watu wengi kuhudhuria mkutano wake mmoja ambapo watu milioni 6 walikusanyikana pamoja kwenye mkutano wake wa injili yaani ni kama Taifa zima la Burundi. Ndugu hii sio ya kukosa kwa wewe uliye Dar es salaam na mikoa ya jirani. ni saa 8 mchana. njoo tumtukuze MUNGU pamoja na tuyashuhudie matendo yake makuu kupitia mwanaye wa pekee YESU KRISTO.
MUNGU akubariki sana.





Comments