USINGIZI WA KIROHO * sehemu ya mwisho.*

NA MTUMISHI GASPER MADUMLA


Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tuendelee…

Dhumuni kubwa la fundisho hili ni kufichua siri iliyopo wakati ulalapo katika usingizi wa kiroho,kwamba pindi unapojisahau kiroho basi,
unampa nafasi ibilisi kukubadilishia kwa kukuchukulia kile kizuri na kukuachia kile kiovu,au kilichokufa kabisa.

Tuliangalia mifano mingi ya maandiko yakituambia kwa habari ya USINGIZI WA KIROHO.

Leo tunaendelea pale tulipokuwa tumeishia katika sehemu ya sita,
Tuliangalia pia namna ambayo Samsoni naye alipolala USINGIZI basi adui zake nao walimshinda.

Tulisoma,
Waamuzi 16: 21 ;
“ Wafilisti wakamkamata,WAKAMNG’OA MACHO ; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.”

Samsoni aliposinzia ndipo adui zake walimuweza ingawa walimuondoa nguvu zake,
tena adui zake wakahakikisha kwamba kitu cha kwanza wanamng’oa macho yake Samsoni,
macho aliyong’olewa yanawakilisha macho ya rohoni,
ili asije kuona tena na akawashinda.

Tena wakamshinda,Biblia inatuambia baada ya kung’olewa macho,Samsoni akapelekwa mpaka GAZA.
-GAZA ilikuwa ni kambi yao Wafilisti,
-GAZA ilikuwa ni ngome ya Wafilisti,mahali ambapo wakubwa wa wafilisti walikuwa huko,
-Gaza ilikuwa ni sehemu ya mateso,Hivyo Samsoni akapelekwa huko,
Tena tunasoma hapo kwamba ( Waamuzi 16:21) baada ya Kumng’oa macho,wakampeleka GAZA,kisha sasa WAKAMFUNGA KWA VIFUNGO VYA SHABA.

Ikimaanisha kuwa sasa Samsoni yupo katika vifungo mahali ambapo hawezi hata kufurukuta kabisa,
tena wakampeleka kusaga ngano.
Ngano aliyokuwa akiisaga ilikuwa ni kwa ajili ya faida yao Wafilisti,
maana hapo alikuwa ni mtumwa wao.

Lakini yote haya yalitokea baada ya kuondolewa nguvu WAKATI ALIPOKUWA AMEJISAHAU AKALALA USINGIZI.
Na hali ndivyo ilivyo sasa,pindi ULALAPO USINGIZI WA KIROHO ujue adui yupo macho tayari kukung’oa macho yako kwamba usishtuke kabisa na hukubaliane naye kwa ile hali;

kumbe !
si hali yako halisi,Pia adui atahakikisha anakupeleka GAZA katika ngome yake,ili ufanyike mtumwa wake,tena hatakuacha ukae bure huko GAZA bali atakupa kazi ya KUSAGA NGANO yaani umtumikie.

Leo hii wapo watu wengi ambao walipokuwa kwa Bwana walijisahau wakalala USINGIZI WA KIROHO baadaye shetani huja na kuwapangia ratiba yake kwamba waifanye,na waliposhtuka tu walijikuta wapo ndani ya ratiba ya shetani maana yeye akikupangia ratiba basi ujue ni lazima utaifanya tu.

*Tazama sasa watu wa namna hiyo walipolala USINGIZI WA KIROHO yaani walipojisahau kufanya mazoezi ya UTAUWA walijikuta wapo ndani ya himaya ya shetani wakimtumikia adui/shetani naye huyo shetani akapanda pando la uharibifu ndani yao.

• Lakini leo ninakutangazia UREJESHO wa mali zako zilizochukuliwa na ibilisi kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti.

• Kila pando lisilopandwa na Mungu baba wakati ULIPOSINZIA KIROHO,leo mapando yote yanakwenda kung’oka
Ubadilishano wa kipepo(Demonic change) katika ulimwengu wa roho upo mpaka hivi sasa.

-Kwa sababu shetani anajua kwamba una mali nzuri ambazo yeye hana.Katika mbadilishano huu shetani anasubiri ULALE KIROHO ili yeye apate nafasi ya kuchukua yaliyo mema na KUPACHIKA yaliyokufa.

Shetani hana jipya,yeye hurudia rudia yale yale yaliyopita
• Tukiwa macho kiroho basi shetani hana nafasi ya kutuibia mali zetu.Maana hata maandiko yanatuambia “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.” Waefeso 6:10

*Wapo watu ambao hapo mwanzo walikuwa safi ki-imani na wanajikuta sasa wakiingia katika maangaiko makubwa pale walipoiacha IMANI
Kuiacha imani ni moja ya KULALA USINGIZI KIROHO.

*Imefika wakati sasa wa kushtuka juu ya mbadilishano uliotokea NYAKATI ZA USIKU.

Nyakati za usiku katika ulimwengu wa roho ni muda ambao falme za giza zikishindana na falme ya NURU
Sasa kwa kipindi hicho kulala ni rahisi sana kwa sababu yakupasa kuongozwa na Roho mtakatifu.

• Je ulikuwa na maisha ya NDO nzuri kipindi ulipokuwa macho kiroho,na sasa NDOA yako haieleweki?yaani unajikuta tu unachukiana gafla na mke au mume wako pasipo hata sababu za msingi?

• Je unasoma lakini uelewi kabisa ukisomacho uwapo shule?
• Je shetani amezuia tumbo lako lisipate mtoto?Au kila unapojifungua mtoto hufariki?

• Je hapo kwanza ulikuwa na IMANI kwa kristo vizuri lakini sasa ujui kilichotokea hata uko mbali na UWEPO wa Bwana ?
• NA MAMBO KAMA HAYO..

*Kwa maana hayo yote ni mabo yaliyoletwa na ibilisi pale ulipojisahau ki-roho,
Maana hata hapo ulipo,ulistahili usiwepo hapo,yamkini ulipaswa uwe mbali kiimani,hata kiuchumi Lakini shetani alikubadilishia na kukupa kilichokufa ambacho ndio hicho ulichonacho hivi sasa.

*Nataka nifanya maombi na wewe,
mawasiliano yangu ni 0655 111149

MWISHO.
UBARIKIWE.

Comments