USINGIZI WA KIROHO * sehemu ya nne *

Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tuendelee…

*Ikiwa makahaba walimuendea Bwana, naye Bwana akaamua kwa haki, JE SI ZAIDI SANA KWAKO WEWE AMBAYE SI KAHABA?...

Haleluya…

*Bwana wetu ambaye ni Mungu mkuu,naye ndiye Mfalme wa Wafalme,
Yeye ambaye hukumu zake ni za haki siku zote.
Kamwe hatakutupa pindi umuendeapo.

Tazama jinsi mfalme Sulemani alivyoamua kesi ile ya makahaba wawili kwa kutumia hekima ya kipekee,
Tunasoma,
1 Wafalme 3:27
“ Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe huyu wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake.”

*Ingawa adui alikuwa akifurahia kwamba wakose wote yule mtoto aliye hai kwa sababu adui siku zote yeye yupo kwa ajili ya kuiba,kuharibu,
kuchinja na kubomoa ( Yoh 10:10 ),

Lakini mfalme akaamua tofauti kabisa na vile adui alivyokudhania ,NA HUYO NDIE MUNGU WETU MWENYE KUTUPIGANIA USIKU NA MCHANA,MWENYE KUTUSHINDIA KESI KWA HAKI.

*Leo hali ilivyo ni kwamba;
Watu wengi wanatumia vitu ambavyo vilishabadilishwa tayari katika ulimwengu wa roho,
wakati walipokuwa wamejisahau na kulala kiroho,adui huja na kupanda pando lisilotokana na Mungu Baba.

Kisha wanajikuta mambo yao hayaendi kama vile hapo mwanzo.Wengi hatufahamu siri hii kwa habari ya UBADILISHANO WA KIROHO/SPIRITUAL EXCHANGE,na tunaona ya kuwa ni sawa tu.

Lakini mimi leo hii ninakuambia si sawa,Mungu hakukuumba hivyo ulivyo sasa,yaani uishi katika hali mbaya ya maisha ya kutozaa kiroho hata kimwili,ipo nguvu iliyotumiwa na adui nyakati za usiku kubadilisha yale mema kwa mabaya.

Biblia iko wazi kabisa juu ya jambo kama hili,Labda tusome andiko jingine ikiwa kama hukunielewa vizuri hapo awali tulipoangalia juu ya mfano wa makahaba wawili.

Hapa tunasoma sasa katika;
Mathayo 13:25-26
“ LAKINI WATU WALIPOLALA, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.”

*Kipindi ambacho watu walipokuwa wamelala ndipo adui uhamka,Biblia inatuambia ,adui akaja na kupanda magugu katikati ya ngano.

*Lengo la adui ni kuharibu ile ngano nzuri iliyopandwa.
* Tufahamu kuwa Neno la Mungu ni mfano wa mbegu nzuri iliyopandwa ndani ya roho yako,
Lakini yupo adui ambaye yamkini ulipolala tu,
yeye akaamka upesi na kuja kupanda magugu katikati ya mbegu nzuri,
ili kwamba ukiamka ukutane na magugu yatakayokuzuilia kushindwa kupokea mambo ya ki-Mungu.

Bwana Yesu anatuelezea vizuri kabisa juu ya mfano wa NGANO na MAGUGU katika Mathayo 13:36-39

*Mwana wa Adamu yeye ndie aliyezipanda zile mbegu njema,
Kisha lile konde/shamba ni ulimwengu,
ZILE MBEGU NJEMA NI WANA WA UFALME,na yale magugu ni wana wa uovu,mstari wa 39 unasema hivi ;

“ yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.”

*adui alitambua siri hii kwamba,
kama akipanda hayo magugu pembeni pembeni ,
basi ang’elijulikana kwa haraka au ang’ejulikana kwa wepesi,
na ndio maana tunaona akapanda magugu KATIKATI YA NGANO kusudi usije ukatambua kwa wepesi mbadilishano huo uliotokea nyakati za usiku ulipokuwa umelala.

*Na hivi ndivyo picha ilivyo katika maisha yetu ya kila siku,yeye shetani hutujia kama malaika wa nuru ili kusudi tusije tukamtambua kwa wepesi.

-Lakini katika ujio wake ibilisimkononi mwake amebeba kitu kilichokuwa ni kiovu kwa lengo la kukubadilishia kwa kile kizuri ulichopokea kwa Bwana pindi utakapo kuwa umelala kiroho.

*Usikose fundisho lijalo,lipo kusudi kwako hata kusoma ujumbe huu,kwa huduma ya maombezi mawasiliano ni 0655 111149

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.
mtumishi Gasper Madumla

Comments