USIRUDIE KOSA LA ESTHER

iky

Yaliyoandikwa kwenye Biblia yaliandikwa kusudi la kutufundisha, kutuelimisha, na ni kitabu cha Mungu mwenyewe.
Wengi mnafahamu ya kwamba Esther alikuwa ni Malikia katika nchi ya ugeni, maana asili yake ni Israel, lakini akawa Malikia katika nchi ya Shushani ngomeni. Esther alifanya kosa ambalo wengi bado tunalifanya leo.
KOSA LA ESTHER: Kusahau kuwa alipata nafasi ile sio kwa ajili yake au nchi ya Shushani ngomeni, bali kwa ajili ya wakati wa taabu ya Israel. Hata alipojua ya kwamba Israel wako kwenye njia kuelekea mauti hakuona inamhusu maana tayari yeye ni Malikia.
Akasahau kuwa amri ya kuuwawa iliwahusu Wayahudi wote, angeponaje na kadhia hiyo wakati na yeye ni Myahudi. Ole wake Esther asingekubali kusimama kwenye zamu yake.
USIRUDIE KOSA: Najua umebarikiwa, umepata kazi unalipwa mshahara, umebarikiwa gari ya kusafiria, tena una chakula vingine wanakula paka na mbwa nyumbani kwako wakati kuna majirani hawana chakula hicho.
USIRUDIE KOSA: Kuinuliwa kwako kuna sababu katika kuujenga UFALME WA MUNGU!
MWL. DANIEL GINGO
REVELATION HOUR MINISTRIES
DAR ES SALAAM - TANZANI

Comments