UTAJIRI SI KITU KAMA MOYONI MWAKO HUNA MUNGU



Luka 12:16 – 21 “16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; 17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. 18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. 19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. 20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? 21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”

BWANA YESU ASIFIWE!
Nawapenda sana, Mungu awabariki wote katika kuri-ishi na kulitenda NENO lake.

Leo nimependa kushiriki nanyi katika neon hili la jinsi ya kujiwekea akiba yako vyema na kuzidi kubarikiwa zaidi na MUNGU. Ni kama hapo awali nilivyoanza na NENO kutoka katika kitabu cha Luka, Tukiona ya kwamba “HAZINA/MALI ZAKO AU ZETU KWA WINGI SI KITU KAMA MOYONI MWATU HATUNA MUNGU au kuwekeza mali na maisha yetu katika hazina ya Mbinguni”

Mali/Hazina tulizonazo wengi ni vile vipawa mbali mbali tupewavyo na Roho mtakatifu si peke yake kuwa na magari, fedha nyingi n.k la hasha.

Kuna mfano wa tabia mbili za matajiri Biblia inatufundisha juu ya neon hilo, TAJIRI MJANJA/MWEREVU NA MPUMBAVU.

Siku zote Mungu akikubariki tujifunze wapendwa kulingana na karama na vipawa tulivyopewa na Mungu kuvitumia/kuwekeza kwake katika kurudisha utukufu kwa na si hasa kuonekana mbele ya wanadamu ili wakutukuze na si kumuinua Mungu kwa matendo mema anayokutendea, ndo mana Luka 12:21, 15, 31 inasema juu ya TAJIRI MPUMBAVU mana alikuwa si mtoaji bali anajirimbikizia mali kwa ajiri ya uhai wake pasipo kujikabidhi mikononi mwa MUNGU “21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu. 15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. 31 Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa.” Ikiwa na maana ufahari na uzima pia utajiri wako hauko hasa kwenye mali ulizonazo na hasa kuwa na choyo bali katika kuzidi kumtafuta Mungu na kukabidhi njia zako mbele zake naye atakuongoza

Pia mfano wa tajiri MJANJA/MWEREVU “Kornelio”
Matendo ya Mitume 10:1-4 “1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, 2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. 3 Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio! 4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.”

Je mpendwa Tujiulize sadaka zetu au matoleo au utajiri wetu kweri unamgusa Mungu hata kutuma malaika kutupatia maono na taharifa tofauti juu ya utajiri wetu? Kuliko kuwa na choyo.

Neno latwambia Zaburi 19:8 “Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru.”

Ewe Mpendwa tuzidi kusimama imara katika vipawa/utajiri Mungu aliotupatia sawa sawa na Neno lake pasipokupoteza kitu mana 1 Wakorintho 3:7 inasema “Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.” TUMWITE MUNGU JUU YA KILA FANIKIO LETU NA KUWEKEZA KWAKE HAKIKA YEYE NDIYE MSTAWISHAJI.
MUNGU AWABARIKI SANA, akufungue Macho yako ya rohoni na hakika kuenenda na Mapenzi yake, tuzidi kuwasaidia wajane, omba omba, wasio na kitu kwa ujumla wote wenye shida ama uhitaji wetu kwa nafasi na viwango tofauti Mungu anavyotubariki kwa utukufu wake

MWISHO TUKUMBUKE: “Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”

Na hakuna utajiri au ngome ya kuasi itakayosimama mbele ya BWANA, Mathayo 12:25 “25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.”

By Edward Tibenda

Comments