WATU WATATU KANISANI

 na Mwl Nickson Mabena


1.Binadamu wa asili
Hajaokoka (MPAGANI), mf katka wanafunzi wa Yesu.. YUDA: Yoh 12:6-
Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema, Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini?  Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo. inaonyesha Yuda alikuwa mwivi kabla ya kumsaliti Yesu.

Mtu huyu wa asili hana nia ya Kristo (1Kor 2:15-16
Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. )
Hawayasikii maneno ya MUNGU (Yoh 8:47
-Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu. )......
--- Hasara ya kuwa mtu wa asili ; Yoh 9:31-

Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. 
 
2.Binadamu wa kiulimwengu..
---sifa zake; Ni mtu wa mwilini (Gal 5:19-21-
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. ), 
 
pia ni mtu wa DINI ( 1kor 3:3-
kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? )

3.Mtu mtakatifu. (Zabur 16:3
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao. ),
--- lakini kwa mtu mtakatifu (2Timoth 3:12
Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. ).

NB. UWEZEKANO WA KUBADILIKA KUTOKA MTU MMOJA KWENDA MWINGINE UPO!!!!!!!.


by Mwl Nickson Mabena

Comments