Zijue Karama Za Roho Mtakatifu – I


Na Mwl. Christopher Mwakasege


I Wakorintho 14:12. Inasema ‘vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za rohoni, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa. Mungu hafanyi kitu bila kusudi, na kusudi la semina hii ni:-
Kuna jambo Mungu anataka kufundisha katikati yetu ambalo litahusisha sana utendaji wa karama za Roho Mtakatifu.
 Kurahisisha ujenzi wa kanisa lake na kazi zake. Mfano, kuna urahisi wa kujenga kwa kutumia mashine za kujengea na kubeba matofali kuliko kutumia mkono, ni sawa na kufanya kazi ya Mungu kwa kutumia karama za Roho Mtakatifu.
I Wakorintho 12:4; anasema pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. Karama si za mtu ni za Roho Mtakatifu na kazi yake ni kulijenga kanisa.
Yesu alisema katika kitabu cha Mathayo 16:18; ”nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitaliweza”. Karama zinatokea mahali kama apendavyo Roho. Katika kitabu cha Yohana 14:16, Yesu alizungumza habari za kutuletea msaidizi mwingine, yaani Roho atakapokuja atachukua nafasi ya Yesu katika kulijenga kanisa lake.
Roho Mtakatifu sio karama bali anazo karama, pia Roho Mtakatifu sio nguvu bali anazo nguvu. Tunda la Roho linapofunuliwa ndani ya mtu tabia ya Mungu hujitokeza kwake.
Katika kutafuta vitu vya Mungu, ili kufahamu karama za Roho Mtakatifu na kazi zake, kuna gharama. Mfano, kwenye ndege kuna first class, business class na third class. Ukitaka kupata huduma nzuri zaidi lazima uongeze pesa (gharama) ili upande business class au first class. Lakini dereva wa ndege (captain) ni yule yule. Vivyo hivyo katika maswala ya Mungu wako wanaokaa first, business au third class, lakini wote tunakwenda mbinguni. Hivyo tunahitaji kuingia gharama ili tukae first class ndani ya Yesu. Gharama hizo ni kama:-
i) kusoma neno la Mungu kwa bidii kwa kadri inavyowezekana ili neno hilo likae ndani yako kwa wingi, maan kujua karama za Roho Mtakatifu bila kuwa an maneno ya Mungu ni vigumu.
ii) Maombi n.k.
I Wakorintho 12:1 inasema ‘basi ndugu zangu kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu’. Tunahitaji kuwa na hamu ya kuona kwamba karama za Roho Mtakatifu zinafanya kazi na zinafahamika. Hamu hiyo imepotea katika kanisa la Mungu na hivyo kufanya kazi ya ujenzi wa kanisa la Mungu kutofanyika kama Mungu anavyokusudia.
I Wakorintho 14:12; ”Vivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.
UTENDAJI KAZI WA KARAMA.
Mambo muhimu (ya msingi) kufahamu ili karama ziweze kufanya kazi. Mambo hayo ni:-
1.) Kubali kuwa karama za Roho zinaweza kufanya kazi kwako pia.
I Wakorintho 12:4.11; ”Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule, lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye”. Roho Mtakatifu ndani ya mtu anazo karama zote bali anamgawia kila mtu kama apendavyo yeye. Rumi 12:3-6; inasema ”kwa maana kwa neema niliyopewa na mwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyo mpasa kunia ……….., basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali …………..”.
2.) Uwe na hamu (haja) kubwa ya msaada wa Mungu.
I Wakorintho:1,12; ”ufuateni upendo na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu, vivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.
Angalizo: karama siku zote zina mvuto.
3.) Tembea katika wito (nafasi) yako.
Warumi 12:6, ”……… kwa kadri ya neema tuliyopewa…”, yaani wito (kiwango) ulichopewa. Ndani ya wito kuwa nafasi ambayo Mungu amekupa. Kuna ngazi, kuna mahali na muda unaotakiwa kuufanyia huo wito. Galatia 2:6-7 ”……walipokwisha kujua neema niliyopewa…….. walinipa mimi mkono wa kuume wa shirika”.
Mfano: kuna tofauti ya karama ya unabii na huduma ya unabii, yaani kila mtu aliyeokoka anaweza kutoa unabii bali si kila mtu ana karama ya unabii.
4.) Karama kutenda kazi vizuri ndani ya mtu inategemea kiwango cha Imani alichonacho.
Rumi 12:6; ”basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali …….. ikiwa unabii tutoe unabii kwa kadri ya imani”. Sio zaidi ya hapo. Rumi 10:17; ”imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo” yaani kiwango cha imani ulichonacho hakiwezi kuzidi hapo. Imani huja tu kwa neno la Kristo. Biblia haituruhusu kutembea kwenye karama zaidi ya imani tuliyo nayo.
Angalizo: kufahamu neno la Kristo kwa wingi ni muhimu. Tembea katika karama za roho kwa kadri ya imani.
Karama zitumike kwa kadri ya Imani yaani utendaji kazi wa karama za Roho Mtakatifu ndani ya mtu utategemea kiwango cha neno la kristo kilichoko ndani yake. Hii ni kwa sababu Mungu alikusudia kuwa karama katikati ya kanisa zifanye kazi kwa ufanisi na usalama ili kulijenga kanisa.
Mfano: Mungu hakuweka unabii ili uongoze kanisa; ila ni kwa ajili ya kuthibitisha neno ambalo Mungu amekwisha kulisema ndani ya mtu.
Kwa sababu karama si zako ni za Roho Mtakatifu, kama huna neno la kutosha ndani yako karama inaweza ikaletwa ndani yako ukaikataa.
I Wakorintho 12:8 ”maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa apendavyo Roho yeye yule”. I Petro 4:10; ”kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana….”. Kuna kupewa na kupokea- karama. Unaweza kukataa kwa kutokuja au hofu n.k.
5.) Jifunze jinsi Roho anavyowasiliana na roho yako, nafsi yako na mwili wako.
I Wakorintho 3:16; ”hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?” Mtu ni roho anayo nafsi na anaishi katika mwili. Roho Mtakatifu pia yuko ndani ya mwili. Hesabu 30:2 ”Mtu atakapo mwekea Bwana nadhiri, ……. Asitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake”. Unaposema maneno yanafunga nafsi yako.
Mwili unatawaliwa na nafsi, nafsi kazi yake ni kutafsiri kile ambacho mwili unasema ili roho ielewe na kile ambacho roho inasema ili mwili uelewe. Kwa hiyo nafsi inasaidiwa pale, unaposoma neno ili iweze kutafsiri mambo ya rohoni sawasawa na neno. Marko 2:5-8, ”naye Yesu, alipoiona imani yao, …….. wakifikiri mioyoni mwao ….. Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao …..”. Galatia 6:17; ”tangu sasa mtu asinitaabishe kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.
6.) Ujazo wa Roho Mtakatifu. Sio wa siku moja ambao unatosheleza.
I Petro 4:9-11 ”mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika, kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama,……….. mtu akihudumu na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu, …….”. yaani kila wakati kuna nguvu fresh, mtu asihudumu kwa nguvu alizojaliwa bali anazojaliwa kila wakati na Mungu. Hivyo tunahitaji kurudi kwa Mungu kila wakati kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Kuna kiwango cha nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya mtu ambacho hakiwezi (kwa kuwa ni kidogo) kusukuma karama fulani ili ziweze kuhudumu au kufanya kazi; ndio maana tunahitaji kujazwa kila wakati.
Usikose Sehemu ya Muendelezo wa Somo hili Siku ya Kesho.

Comments